KERO CCM na serikali yenu kuandikisha watoto wawapigie kura mnaweza, ila kuhakikisha tunapata huduma za muhimu kama maji Aaaaa!

KERO CCM na serikali yenu kuandikisha watoto wawapigie kura mnaweza, ila kuhakikisha tunapata huduma za muhimu kama maji Aaaaa!

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mawele

Senior Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
119
Reaction score
320
Kuandikisha watoto ili kuiba kura mshinde muunde Serikali mnaweza, mna kila mbinu za wizi wa kura ili muongoze ila hamna mbinu za kutatua changamoto za mnaolazimisha kuwaongoza.

Au akili huishia kwenye kuchakachua? Miaka 60+ bado tunaongelea uhaba wa Maji Tanzania, Dar maeneo mengi maji hakuna, Malamba maji yametoka mara moja na mwezi umepita sasa, mabomba mnadhani yapo kwa ajili ya kupigia picha? Maana hayatoi maji ila kuiba kura mna juhudi sana.

Kweli Maji tu yanawashinda? Nchi mnataka mpewe mfanye kitu gani tena? Iwapo kitu kama maji kinawashinda licha kuwa nchi ina vyanzo vingi vya maji, yaani hamjui mnatafuta nchi ya nini labda ili muifuje maana kuindeleza ishawashinda.

Dar imekuwa ya madumu, watu wanachota maji ya mitaroni ila mpo tu kazi kusifia ooo kafanya hiki kafanya kile kipi wakati hatuna maji miezi tunahangaika na madumu na mandoo.

CCM hovyo kabisa hamna maana kabisa.

Pia soma:

KERO - Morogoro: Wananchi wa Mindu hawana Huduma ya Maji, wanatumia ya kwenye makorongo

√ - Waziri Aweso: Maji yapo, aagiza wafanyakazi wa DAWASA kutokaa ofisini "Wananchi wanahitaji maji"
 
Back
Top Bottom