kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Watoto wadogo wanapolia kwa kuchokozwa na mtu mzima au hata kwa kuchomwa sindano, ili kumnyamazisha asilie mzazi atamuuliza mtoto swali la kizushi la "nani mchokozi?". Mtoto atasema yule pale, na mzazi atamwambie tema tumpige, na mzazi atampiga kizushi huyo mchokozi, na mtoto atanyamaza kwa kuamini yule mchokozi wake amekiona cha mtema kuni.
CCM inatuchezea shere kwenye mambo mengi sana na kutufanyia ileile ya tema tumpige kama watoto. Mwenyekiti wa CCM ndiye Mkuu wa nchi na mkuu wa serikali, mawaziri wote na 99% ya wabunge wote ni CCM. Hakuna mswada wala sheria itapitishwa bila CCM kufahamu na kushirikishwa kupitia Mwenyekiti wa CCM, mawaziri, na wabunge wa CCM.
Mfano, haiwezekani kusikia eti CCM haina habari na tozo kwa wananchi. CCM inataka kujitenga na malalamiko ya tozo kana kwamba haifahamu kilichofanyika na kinachofanyika kwa kuikemea seikali wakati mwenyekiti, mawaziri na wabunge wa CCM ndio waliopitisha tozo hizo, sheria na kanuni zote nchini tangu nchi ipate uhuru.
Binafsi ninajisikia kichefuchefu ninapowaona akina Kinana na Shaka wanazunguuka huku na huko wakifanya "tema tumpige" kwa wananchi mazuzu. Wanajifanya wanaishangaa serikali yao mbele ya wananchi kama vile walikuwa wamesafiri wakati serikali na bunge wakipitisha sheria na kanuni mbalimbali zinazowaumiza wananchi. Wanajifanya wanaikemea kizushi serikali yao ili kuwanyamazisha wananchi wanaolalamika dhidi ya sera za CCM zinazotekelezwa na serikali zao, yaani TEMA TUMPIGE.