Heri Amani
New Member
- Dec 14, 2011
- 1
- 0
CCM na Udini ni mojawapo ya mada ya Wana JF iliyonifurahisha sana. Ni kweli kabisa chanzo cha tatizo ni kile Mchambuzi ameita "obwe la dini ya kiraia" baada ya Serikali ya CCM kuachana na Sera ya uchumi wa Ujamaa na Kujitegemea na kukumbatia Sera za soko huria. Hali hii imeleta "ideological vacuum" na si "ombwe la uongozi - Leadership vacuum" kama ambavyo Watanzania wengi wanavyofikiria. Hivyo suluhisho la kweli la uchochezi wowote ndani ya nchi yetu ni pale tu Taifa litakapojenga itikadi ya kitaifa itakayoleta mshikamano ndani ya jamii zote. Janga linaloinyemelea nchi yetu ni kwamba hakuba chama chochote cha siasa kinachohangaika kujenga itikadi (ideology) itakayowaunganisha Watanzania wote chini ya mfumo wa soko huria. Vyama vyote vimebaki wanapigania madaraka ya dola huku kukiwa hakuna chama kinachoshughulikia elimu ya itikadi ya kitaifa ili kuziba ombwe lililopo. Tatizo hapa si miradi ya maendeleo au kugawana keki ya kitaifa kwa usawa. Tatizo ni kitu gani kitawaunganisha Watanzania wote katika mfumo wa soko huria ambao kwa asili yake (nature) ni lazima kuzaa matabaka ya walio nacho na wasio nacho? Utaona ya kwamba walio nacho na wasio nacho si rahisi kukaa pamoja bila kwanza kuwa na itikadi inayowaunganisha. Ndipo hapa tunaona mambo ya udini, mambo ya kikanda, mambo ya kizawa, mambo ya ukabila, na kadhalika. Je, zoezi la kuunda Katiba Mpya inaweza kuwa fursa nzuri ya kutuondelea "ombwe la kiitikadi ya kitaifa na hivyo kuwa mwanzo wa kujenga itikadi itakayojaza ombwe lililopo? Tusubiri tuone.