tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
CCM walianza na ngonjera ya Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania. Baada ya kuimba ngonjera hii kwa muda wa miaka 5 na kukosa muitikiaji, wakaamua kubalili mapigo na kuibuka na ngonjera mpya waliyoipa jina la Ari Mpya, Nguvu Mpya na Kasi Mpya (ANGUKA) na kumalizia na ngonjera ya Hapa Kazi Tu na sasa eti wanatuambia Kazi Iendelee! Pamoja na usanii huu wote, maisha ya mtanzania yamezidi kuwa duni mwaka nenda mwaka rudi!
Tangu CCM washike madaraka nchi imekuwa haina mwelekeo. CCM inafanana na mtu mwenye jino moja. Mtu kama huyo hata umlishe namna gani hawezi kunenepa. Lazima atakufa kwa njaa kwa kuwa hana meno ya kutafunia chakula.
Nchi hii imejaliwa rasilimali nyingi za asili kama vile ardhi, maziwa , bahari na mito, madini, misitu, wanyama, nk. Lakini kwa kuwa CCM haina meno, imewaalika wenye meno (wawekezaji) waje watafune (wakavune) rasilimali hizo huku wakiiacha nchi ikiwa ikiwa tupu! Migogoro katika maeneo ya uchimbaji madini na maeneo yenye ardhi ya rutuba imekuwa ikitokea kila kukicha. Wananchi wamenyanganywa ardhi yao nzuri wamepewa ‘wawekezaji'. Watanzania wanyonge wamegeuka wakimbizi ndani ya nchi yao. Wananchi wamekata tamaa na utawala wa CCM. Hawana hamu nayo!
Huduma za jamii kama vile maji, umeme, barabara, elimu na afya imekuwa duni kiasi cha kukatisha tamaa. Wanafunzi kusomea chini ya miti ni suala la kawaida kabisa na wale wachache waliobahatika kupata madarasa duni huketi chini ya sakafu ya vumbi au juu ya matofali! Hali hii mpaka lini hasa? CCM wala hawajali kwa kuwa watoto wao husomeshwa kwenye shule nzuri zenye walimu weledi na vifaa vya kufundishia vinavyotosheleza mahitaji.
Mwalimu Nyerere alipokea uongozi wa nchi kutoka kwa wakoloni wakati nchi ikiwa taabani kiuchumi lakini hatukuwahi kushuhudia ugumu wa maisha kama tunavyoshuhudia hivi sasa. Ni lini hasa CCM na mafisadi wake wataboresha huduma za jamii na kuwafanya wananchi waishi maisha yenye utu?
CCM haina tofauti na mtu mzima aliyekabidhiwa kumlea mtoto mdogo badala yake akanywa maziwa ya mtoto na kumuacha mtoto akifa kwa njaa.
Hii maana yake ni kwamba CCM imeamimiwa na wananchi wakaikabidhi rasilimali zote wakitegemea iwaletee maendeleo lakini wanaonufaika na rasilimali hizi ni mafisadi wachache ndani ya chama na serikali huku wananchi wakiishi maisha duni kupindukia.
CCM ni sawa kabisa na mtu mzima anayemtumia mtoto mdogo kama ngazi kwa manufaa yake binafsi. Mtu wa namna hiyo lazima anakuwa na hililafu kichwani mwake.
Vivo hivyo, CCM na mafisadi wake huwatumia walalahoi kama ngazi ya kupandia madarakani na wakishayapata hayo madaraka huuwaacha wananchi solemba. Sote ni mashahidi jinsi ambayo CCM inavyowakumbatia mafisadi na makuwadi wa mabeberu wanaokomba rasilimali za taifa na kuiacha nchi ikiwa kama jangwa.
CCM wameishiwa ubunifu wa kuitoa nchi hapa ilipo na kuipeleka mbele. Hata mcheza shoo anawazidi akili maCCM. Mcheza shoo hutumia mwili wake kama rasilimali ya kujiletea maendeleo kwa kuwaburudisha wateja wake na kuwakonga nyoyo zao.Kama vile mcheza shoo anayotumia rasilimali aliyonayo (mauno) kujiletea maendeleo, tulitarajia kwamba CCM watumie rasilimali zilizopo nchini kuwaletea wananchi maendeleo endelevu lakini wao bado wamelala usingizi wa pono.
Hata mbuzi anawazidi CCM akili. Wakati wa kiangazi, mbuzi hutumia maarifa yote kuyafikia majani popote yalipo lakini CCM wao wamelala usingizi huku wakitegemea kuombaomba misaada badala ya kutumia rasilimali tulizonazo kuwanufaisha watanzania wote.
Nchi hii ina rasilimali lukuki ambazo kama zingetumika vizuri zingeleta manufaa kwa watanzania wote. Kinyume chake rasilimali zote wamekabidhiwa mabeberu (wanaopambwa kwa jina la ‘wawekezaji') ambao wamemimika kutoka kila pembe ya dunia na kukimbilia kuvuma utajiri uliojaa tele nchini Tanzania.
Baada ya CCM kushindwa kuiendeleza nchi, wameamua kuwarubuni wananchi wenye njaa kwa lengo la kuwarejesha madarakani kila uchguzi mkuu uitishwapo. Mgao wa fedha wanazopata kutoka kwa mabepari waliowakabidhi rasilimali zetu, hutumikia kama chambo cha kuwarejesha madarakani kwa kuwapikia chakula, kuwapanga kama ng'ombe kwenye mistari na kuwalisha pilau.
View attachment 175933
Hii ndio kete ya mwisho iliyobaki. Mbinu nyingine zozote ziwazo zimeshindwa kufanya kazi. CCM wamewatia wananchi njaa kwa kutapanya rasilimali zao ili iwe rahisi kuwarubuni kwa kuwalisha chakula, kuwanunulia mbege, mataputapu, t-shirts, kanga, fulana, chumvi, sabuni, nk.
View attachment 175929 View attachment 175930
Na kwa kuwa wananchi hawa wana njaa ya kutisha huamua kugawa kura zao kwa CCM, kisha hukaa na njaa na dhiki zao kwa miaka mingine mitano. Miaka mitano ikiisha CCM huwaendea tena na kuwalisha chakula na kuwapa vizawadi uchwara na hatimaye huwarejesha madarakani tena. Huu ni mzunguko hatari sana ambao kama usipodhibitiwa, wanachi wetu watazidi kutopea kwenye ufukara hadi Yesu atakaporudi. Wakati wa kutafuta kura kwa wananchi, wataingia hadi kwenye mahandaki lakini wakishapata hizo kura hawawakumbuki tena wananchi waliowapa kura.
View attachment 175928
Janja ya CCM ni sawa na mfugaji mpumbavu ambaye hamlishi ng'ombe wake lakini kila uchao utamkuta amening'inia kwenye chuchu akimkamua maziwa. Yuko radhi kukamua mpaka damu zitoke kuliko kumlisha na kumnenepesha ng'ombe wake ili apate maziwa mengi zaidi.
View attachment 175926
MaCCM hawaboreshi maisha ya wananchi lakini kila mwaka hupandisha kodi za bidhaa na huduma na kuyafanya maisha ya walalahoi yawe magumu zaidi. Kila bajeti isomwapo utasikia bia, soda, mkate, mafuta na bidhaa zingine zikipanda bei wakati uchumi wa watanzania bado upo pale pale!
View attachment 175924 View attachment 175925
Silaha ya mwisho kabisa waliyosalia nayo ni kuwabeba wananchi kwenye malori ya mchanga kuwapeleka kwenye mikutano yao ya siasa pamoja na kuwalipa posho uchwara ili kuwajazia mikutano yao ambayo siku za nyuma ilikuwa ikikosa wasikilizaji/wahudhuriaji. CCM wametufikisha hapa tulipo baada ya kuwafukarisha wananchi ili iwe rahisi kuwatawala.
View attachment 175958
Posho zenyewe wanzopewa ili kuhudhuria mikutano ya CCM huwa ni kidogo sana kiasi cha kupelekea wahudhuriaji kupigana ngumi na mateke wakigombea hayo makombo kidogo wanayoambulia kutoka kwa mafisadi. Hii ndio CCM zaidi ya mnavyoifahamu. CCM oyeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!
:israel: