Ccm ndiyo wanao ufunguo wa katiba mpya ila wakiteleza wataijutia nafasi hiyo daima

Ccm ndiyo wanao ufunguo wa katiba mpya ila wakiteleza wataijutia nafasi hiyo daima

MUWHWELA

Senior Member
Joined
Oct 26, 2013
Posts
167
Reaction score
238
Salam wanajopo,

mimi binafsi siamini kabisa kama tutaipata katiba mpya inayokidhi haja ya watanzania kwa speed hii tuliyonayoo,kwa nini siamini leo hii hakuna mtu anayeelewa ajenda ya siri waliyonayo wanachama wa ccm waliopitisha mswaada ule wenye utata bungeni ukiachana na hawa wana ccm ambao nao pia wanaunga mkono baadhi ya hoja nzito zilizopo katika rasimu hii ya bwana warioba.

kwa jinsi ambavyo mambo yanakwenda kuna mambo ambayo yanaashiria kabisa kwamba ndani ya bunge maalumu la katiba kutakuwa na mvutano mkubwa,ambao utajenga mpasuko mkubwa sana katika taifa na hili ningependa kuwatahadharisha wanaccm ambao ndiyo watakuwa wengi katika bunge hilo.

chonde chonde wanaccm simamieni mambo ambayo watanzania wote wanayataka ,selikali tatu,chombo cha kuratibu uteuzi,na hoja nyingine nyingi ambazo ninyi mnapingana na watanzania waliowengi,

kitendo cha kuacha kusimamia hilo,hakika nawambieni ccm pamoja na mwenyekiti wenu mtaliingiza taifa katika machafuko,serikali yenu itaparaganyika na kila mtu ataangalia masilahi yake na uhai wake katika uchaguzi ujao.

kama hamulielewi hili leo nawambia,ccm hamna tena ushawishi mkubwa kwa wananchi masikini,ccm ya leo ni ya matajiri kwa hiyo mkiacha upinzani watoke tena nje ndani ya bunge hilo la katiba,,,,siamini kama mtaweza kuuzima tena moto huo..

kwa hiyo tafadhali ndugu zangu tupitisheni salama katika daraja hili takatifu maana mkiteleza mwenyekiti wenu ataenda uholanzi kujibu mashitaka pamoja na viongozi wengine waandamizi,kwa binadamu yoyote makini hawezi kuombea hilo litokee bali tunawaombea pia mpewe hekima na busara ya kutosha kuvumilia kukosolewa,

asilimia kubwa ya hoja zenu si za kitaifa kwa hiyo zitapingwa sana katika bunge hilo ila tunawaomba mvumilie ili tupite salama katika daraja hili...


nawaombea kwa mungu wetu,awatie nguvu na uvumilivu huo ndugu zangu na viongozi wangu wandamizi wa selikali ili ushinde ubaki ccm kwmba serikali yenu ilileta katiba kuliko kuleta machafuko..


NAOMBA KUWASILISHA HOJA
 
Back
Top Bottom