CCM NGOMA MZITO: waitisha kikao cha siri usiku kidhibiti wabunge wao

CCM NGOMA MZITO: waitisha kikao cha siri usiku kidhibiti wabunge wao

PISTO LERO

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2011
Posts
2,819
Reaction score
1,455
Dodoma. Hofu imetanda kuhusu uwezekano wa kuvunjika kwa Bunge Maalumu la Katiba, kutokana na hatua ya CCM kutumia wingi wao kutaka kupitisha utaratibu wa kupiga kura za wazi.

Baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo, wameshauri njia pekee ya kunusuru mchakato huo ni kwa CCM kukubali kukaa meza ya mazungumzo.

Wakati wajumbe hao wakitoa angalizo hilo, taarifa zilizopatikana jana mjini Dodoma zilisema CCM, wameitisha kikao cha dharura cha wajumbe wake wote leo saa 8:00 mchana kwa agenda ambayo bado ni siri.

Habari hizo zinadai kuwa wajumbe ambao ni Wabunge na Wawakilishi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wametumiwa ujumbe mfupi wa simu (SMS) wakitakiwa kuhudhuria kikao hicho bila kukosa.

“Mambo muhimu yatajadiliwa, Mwenyekiti wa Cocas (umoja wa wabunge) anasisitiza mhudhurie bila kukosa, mahudhurio yatazingatiwa,” unasomeka ujumbe huo ambao gazeti hili limeuona.

Baadhi ya wabunge wa CCM hususan wanaotoka Kanda ya Ziwa wanaounga mkono kura ya siri, walidai kuwa kikao hicho huenda kina nia ya kuwatisha ili walegeze msimamo wao.

“CCM wanaogopa kura za siri kwa sababu moja tu, wakiiruhusu watakuwa hawana control (udhibiti) wa wajumbe kutoka Zanzibar ambao wengi wanataka Serikali tatu,” alidokeza mbunge mmoja ambaye hata hivyo, hakutaka jina lake litajwe.

Mbunge huyo alisema kwa tathmini yake, kama utaratibu wa kura za siri utapita, karibu asilimia 80 ya wajumbe wote kutoka Zanzibar, watapiga kura ya kupitisha rasimu ya muundo wa Serikali tatu.

“Kwa hiyo CCM haitaki kabisa utaratibu wa kura za siri, wanataka kura za wazi ama kura ya dhahiri ili waweze kuwa na udhibiti wa wajumbe ili tusitoke nje ya msimamo wao,” alidai mbunge huyo.

Hata hivyo, wakati CCM ikishikilia msimamo wa kura za wazi katika kupitisha rasimu hiyo, wabunge wake wengi wa Tanzania Bara na wale wa Zanzibar wanataka upigaji wa kura za siri.

Akizungumza na gazeti hili jana, James Mbatia alitahadharisha kuwa msimamo wa CCM kulazimisha kura za wazi, siyo kuwatendea haki Watanzania na huenda ikawa chanzo cha machafuko na kukwama kupatikana Katiba Mpya.

“Kulazimisha matakwa ya CCM badala ya wananchi itakuwa ni chanzo cha machafuko na Watanzania hatuko tayari kwa machafuko wala kuona damu ya Mtanzania inamwagika,” alisema Mbatia.
 
na jk naye kaingia dodoma usiku akitokea kwenye msiba wa prof kazaura
 
Huu mkqkati uko wazi jinsi unavyopigiliea misumari na wabunge wa CCM kwa hoja ambazo hazina mashiko. Ni agenda ya iliyo nyuma ya pazia kutaka masuala ambayo wana masilahi nayo yapite kwa urahisi kwa kuanzia na hili la kuwabana wabunge wao wapige kura wanazozifahamu
 
CCM hawajitambui na hawajui nini wanafanya!
Ivi kikwete alitegemea nini alipotaka katiba irekebishwe?
...
Kura za siri ndio mfumo mzuri na kinyume chake ni kukiuka misingi ya kidemkrasia!
Na serikali tatu ni afueni ya Muungano, kinyume na hapo tutegemee machafuko!
CCM hamjielewi!
 
Back
Top Bottom