Elections 2010 Ccm ni chama cha udaku?

Elections 2010 Ccm ni chama cha udaku?

masasi

Member
Joined
Aug 3, 2010
Posts
48
Reaction score
0
Sasa naona ccm wameamua kuhamishia kampeni zao kwenye magazeti
ya mwanachama wao shigongo kama ijumaa,risasi,champion,magazeti ambayo yanawadharirisha mama na dada zetu kwa habari zao za kupikwa,sasa inajdhihirisha wazi kuwa hiki ni chama cha wadaku,wafitini,mafisadi,tuamkeni na tuiwaamshe wenzetu,muda wa mabadiliko ni sasa
 
Siku nyingi CCM imeshakuwa chama cha udaku
 
CCM ni chama cha kisanii zaidi kuliko siasa, uwongo,udaku,umbea, fitina, majungu,siasa za maji taka,ufisadi,uhuni,ubadhirifu na kila aina ya uovu unapatikana CCM.Magazeti ya Shigongo yameleta maafa kwenye jamii nyingi hapa nchini,ndoa nyingi zimevunjika kutokana umbea wa magazeti ya Global Publishers. Sasa kwa CCM kukimbilia huko ni ishara mbaya kwao kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu. Sijui Watanzania wanahitaji ishara gani zaidi juu lichama hili ccm.
 
Siku nyingi CCM imeshakuwa chama cha udaku

Mwangalie Mgosi Makamba
Huyu ni zaidi ya msanii, bingwa wa kubwabwaja na mwepesi wa kuropoka. Nakumbuka kipindi fulani aliwahi kutoa kauli hii mbele ya Mwenyekiti wake wa taifa, nanukuu: "... siasa ni mchezo mchafu ni sawa na mtu kukumwagia kinyesi na ikitokea hivyo unapaswa kukitoa haraka kinyesi hicho toka kwenye nguo zako na kumrushia yule aliyekutupia"

Je, kwa kiongozi kama yeye kutoa kauli kama hii mbele ya mkuu wake na wale anaowaongoza si usanii?

Chama kilikuwa Chama enzi zile za akina Horace Kolimba (RIP) na kina Philip Mangula, siyo sasa kwani kila mtu ni msanii. Hebu ona ahadi hewa za JK huko; Kagera, Rukwa nk anatoa ahadi hazipo hata kwenye ilani ya CCM. Swali je, katumwa na nani? na kwakuwa Chama ni cha kisanii, no one will question on this.

Hapa wakulaumiwa si viongozi ni wanachama na hasa wa-tz wote kwa ujumla wao na hasa wapiga kura.
 
Back
Top Bottom