MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,252
- 8,003
Haiwezeki na haiingii akilini kwenye heka heka za Chaguzi karibia zote za marudio zinazoendelea nchini kila kata wagombea udiwani wa CCM wanapita bila kupingwa, kwani Upinzani wameanza kugombea leo? Mwanzo walikua wanafanyaje?
Watu wanaporwa form mchana kweupe na wasimamizi wa uchaguzi wanatazama, watu wanatishwa na wasimamizi wa uchaguzi wanatazama. Mbona miaka ya nyuma hali hii ya hovyo kabisa haikuwepo, kwanini ni sasa? Hivi hawa watu wanalitaka nini taifa?
Ifikapo kuanzia 2019 kwenye uchaguzi za serikali za mitaa hali inaweza kua tete kuliko ilivyowahi kutokea tangu nchi ipate Uhuru, CCM wanataka kulazimisha mambo kwanini?Hatima ya kutumia nguvu na kunyanyasa watu ni ipi? Tunataka kuelekea wapi?
Binafsi napenda tu niwashauri CCM kua hali ikiwa tete wao ndio watajibu na watakua chama cha kwanza kukimbiwa na watu na kufa kabisa, baadae watajibia haya. Wasione fahari watu kufanyiwa haya, wafurahie katiba iliyopo lakini watambue kua katiba hii hii ambayo hawataki mabadiliko yake ndiyo baadae itageuka kua shimo lao.
Najiuliza, je, upinzani nao wakiamua kusema na sisi hatutaki hali itakuwaje? Hivi CCM wanadhani upinzani wanamuogopa mtu au ni uvumilivu tu ambao unatumiwa na viongozi wao wa juu? Tunafikiri huu uvumilivu wa kina Mbowe,Zitto na wengine hautakua na mwisho? Ikifika mahali nao wakiwaambia wafuasi wao sasa inatosha itakuwaje?
Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama itafika mahali vitasimama katika haki, itafika mahali vitajali raia wao kwa misingi ya katiba ya nchi, watazingatia yale yatakayolinda utulivu wetu. CCM wasifikirie hivi vyombo ni vyao kwa Mtazamo wa Hussein Bashe,hivi vyombo ni vya umma kama ilivyo wao pia wana ndugu walioko upinzani.
Haiwezekani kusema eti Kiongozi flani anafanya mambo makubwa eti ipelekee wagombea wa CCM wapite bila kupingwa, kwani Upinzani wameanza kushiriki uchaguzi leo kiasi kwamba wawe ni watu wa kukosea tuu?Ipo shida kubwa sana tuu, trust me wallah muda utanena.