CCM ni nani katika Watanzania!!NCHI ni ya Watanzania sio CCM

CCM ni nani katika Watanzania!!NCHI ni ya Watanzania sio CCM

Adharusi

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2012
Posts
14,422
Reaction score
7,350
Nimekuwa nikishangaa kama mwananchama wa chama cha mapinduzi,katika swala la katiba mpya,Viongozi wa chama wamekua mbele kung'ang'ania tena majukwaani kuwa Msimamo wa CCM ni serikali mbili,wakati zaidi 60% ya watanzania wanahitaji serikali tatu!huu ni upuuzi,kuamini CCM ni zaidi ya Watanzania,ni kujidanganya tu,Je kila chama kikiamua kupita majukwaani na kutumia vyombo vya Habari kusema kuwa msimamo wetu ni huu,je tutafikia muafaka,huu ni utoto unaoletwa na kina @Nnauye na wenzake.
Binafsi nimechoka hizi kauli za CCM za kuona Warioba katumia bure Fedha za watanzania kukusanya Maoni,kutaka maoni ya CCM yawe mbele na Ya watanzania yawe nyuma.
Angalizo kama CCM itaendelea na utaratibu huu naomba vyama vya siasa vyote vipite majukwaani,vyombo vya habari kung'ang'ania Misimamo yao,hakuna chama kisicho kuwa na Misimamo yake bali wameamua kukubali maoni ya watanzania kupitia Tume ya katiba ya Warioba
""Allah nakuomba usikie maombi ya wengi ya serikali tatu,CCM na maombi yao ya serikali mbili washindwe na kulegea""""
 
Ifike sehemu Wanasiasa waheshimu watanzania wengine!ishu ya katiba tuachiwe wananchi
 
Viongozi wa sisiem wamedhihirisha ufinyu wa mawazo yao. Hata mawe yanatushangaa kukubali viongozi wa namna hii. Haiingii akilini leo CCM wanasema wanataka katiba ya serikali mbili zilizoboreshwa wakati wamekaa na serikali hizo kwa miaka 50 bila kuweza kuziboresha!!!! Hivi kweli kwa mtu mwenye akili timamu anaweza kusimama jukwaani na kuwaeleza watu kuwa pamoja na kero zote za muungano zinazosababishwa na muundo wa sasa wa serikali mbili bado hatuna haja ya kubadilisha muundo huo? Kwa kweli hii ni dharau kubwa kwa watanzania kuona kwamba ni wajinga kiasi hicho hata wanaokwenda kuwasikiliza sio dhambi kusema kuwa ni wajinga. Cha kushangaza hawana hoja ya msingi zaidi ya kusema kuwa wao ni waumini. Hivi kweli tunahitaji katiba ya imani au inayotoa dira ya mustakabali wa taifa hili. Imetosha inachosha usanii wa CCM sasa basi.
 
Kauli ya CCM ndio kauli ya watanzania, Msimamo wa CCM ndio msimamo wa watanzania.
 
Back
Top Bottom