Uchaguzi 2020 CCM ni waoga na Uchaguzi

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2012
Posts
602
Reaction score
2,506
Nipende kuchukua fursa hii kuwapongeza Vijana wenzangu mnaomkubali Tundu Lissu kwani mpo vizuri kiakili, kifikra na mna nia njema na maono makubwa kwenye nchi hii.

Point to note:
Zingatia hii aanda kadi yako ya kupiga kura kama unavyolithamini Tumbo wakati wa kula. Tarehe 28.10.2020 umpigie Tundu Lissu kikamilifu kabisa.

Pili, pole kubwa kwa vijana wenzangu mnaomsifia JPM kwa maslahi ya Pesa na mambo mengine hasi.

Tatu, vijana wenzangu Ifikie mahala Tujitambue tuupanue ubongo. Vijana wengi tunaishi Maisha ya shida, maisha yenye changamoto ambazo huwezi kuzielezea kwa siku 1 labda wiki nzima, vijana wengi tunaishi Maisha magumu tukitegemewa kuondoa mzizi wa umasikini kwenye Familia zetu, ama kwenye koo zetu.

Mfano mwepesi tu Elimu ya Tanzania tunasoma kwa kukopeshwa kweli inaingia akilini.

Wafanyabiashara wengi Tunatozwa tozo zenye ufisadi na Rushwa kem kem.

Ukitaka kupima kuwa Hali ya maisha ni ngumu mfano mwepesi kabisa angalia vifurushi vya mtandao, angalia malipo ya kifedha utapeli na wizi ndio umekithiri.

UJINGA mwingi unafanywa wazi wazi kabisa alafu tunakalia kusifia upuuzi.

Swali jepesi kabisa Awamu hii ya Tano imekusaidia nini katika maisha yako ya kawaida kumbuka umelipa Tozo, kodi na mambo mengine mengi. Swali fupi, Ndege zimekusaidia nini. Hii Awamu ya5 kupitia sera ya Viwanda, kupitia viwanda umenufaika nini maana ajira ni tatizo sugu.

Kwa utafiti nilioufanya hivi karibuni, Watanzania Wengi wanaishi maisha Magumu Sana. Yale mahitaji muhimu ya binadamu tutaishia kuyasoma kwenye madaftari, kutokana na ujinga wa maamuzi tuliyonayo.

Vijana wenzangu popote mulipo mshawishi mtu yeyote mwenye weledi mkubwa akampigie kura Tundu Lissu.

gmfalamagoha85@gmail.com
 
Huyu sikteta amefeli pakubwa. Hakuna atakayerudia makosa kuchagua kiongozi dhalimu kama Meko.

Muda huu niko hapa Kiluvya alipozuiliwa Tundu Lissu. Kuna maelfu ya watu wamekusanyika hapa lakini wote wanamlaani Meko na CCM yake.

Lissu ndiye rais ajaye, amini msiamini.
 
Kabisa, ujinga wa vijana wengi unakinufaisha CCM sana na sasa wanatumia nguvu zaidi kuwahi kuonekana kwani wanajua watu wamechoka sana na mambo yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…