CCM: Nini ubaya wa REFORMS zinazodaiwa na CHADEMA?


kwa sababu ni takwa la kichama badala ya kua la kinchi, lakini pia kuna tafauti kubwa kati ya harakati na siasa
 

Chama kikishakaa madarakani muda mrefu hupoteza nguvu yake ya ushawishi hasa kwa kizazi kipya. Na sehemu kubwa makada wake hukitumia chama hicho kujiunufaisha binafsi.

Iko hivi, ccm sio chama cha kizazi hiki, hivyo haiwezi kushinda itakavyo iwapo kutakuwa na mazingira sawa ya ushindani. Hivyo wanaogopa mabadiliko yoyote ya sheria hasa za usawa kwenye ushindani ni hatari kwa yenyewe kuwepo madarakani. Ccm wanasema wana wwnachama 13m, hilo si kweli maana wamebobea katika kupika data. Ccm itakuwa imeuza kadi 13m, na wala sio 13m wanaoikubali ccm. Hakuna uwezezakano wa ccm kuwa na watu zaidi ya 5m wa kuwapa kura, wakati wao wanataka kwa sasa watangazwe washindi zaidi ya 10m+.

Uchaguzi wa 2010 na 2015 ccm ilijaribu kidogo kutaka kujipima inavyokubalika. Matokeo yote yalionyesha ushindi wa ccm kushuka kwa kasi. Nadhani uongozi wa ccm wakijifungia na kuona hawana uwezo tena wa kushindana kuhalali na kushinda watakavyo, ama hata wanaweza kutoka madarakani, jambo ambalo litakuwa fedheha kwa chama hicho. Magufuli akakibidhiwa jukumu la kuua upinzani. Ndio tukaanza kuona chaguzi za kishenzi kupita maelezo, huku taasisi zote za kimamlaka zikitumika kuua kiitwacho upinzani. Anachokifanya mama Samia sasa ni muendelezo wa ajenda hiyo ya ccm ya kutokomeza upinzani. Hakuna uwezo wa ccm kukubali reforms zitakazowapoteza. Kama huamini hiki si kizazi cha ccm, wakubali reforms upate mrejesho.
 
Kwa takwimu zipi, CCM itashindwa na CHADEMA? CCM ndio maisha ya wananchi ya kila siku, huku tunakoishi mitaani, wananchi wote wanaona mabalozi wa CCM ndio viongozi wao karibu zaidi na hawa ndio wanaowahimiza wanachama wa CCM kwenda kupiga kura.
Ccm haitegemei kura. Ingekuwa inategemea kura ingekuwa kaburi moja na KANU ya Kenya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…