CCM nipe uwezo nitangaze Ujamaa Tanzania kote

Ngoja tukupigie mkuu jitihada zako zimeonekana.
 

..ni kweli wananchi wanatakiwa waipende nchi yao, lakini pia nchi nayo au serikali inatakiwa ionyeshe mapenzi kwa wananchi.

..sisi tulipokuwa vijana tulikuwa na uzalendo kwa nchi yetu kwasababu tulikuwa tunatendewa haki, na tulikuwa na matumaini ya kutimiza ndoto zenu hapa nchini ilimradi tufanye kazi kwa bidii.

..usitegemee kabisa uzalendo ktk nchi ambayo haki zinabinywa, umasikini unaongezeka, ukosefu wa ajira haushughulikiwi, ajira za serikali hazina heshima, elimu haina thamani, n.k n.k
 
Nimekuelewa Sana kiongozi, [emoji120][emoji120][emoji120].
 
Tangaza Ujamaa kwa familia na ukoo wako inatosha, mambo ya Tanzania nzima achana nayo.
 
Tangaza Ujamaa kwa familia na ukoo wako inatosha, mambo ya Tanzania nzima achana nayo.
..huyu bwana mdogo siyo mjamaa wa kweli.

..angekuwa mjamaa kwelikweli asingesubiri kuwezeshwa/kulipwa ili kuutangaza.

..na viongozi wa ccm anaowaomba wamuwezeshe kutangaza ujamaa wenyewe ni makabaila na mabepari uchwara.
 
..huyu bwana mdogo siyo mjamaa wa kweli.

..angekuwa mjamaa kwelikweli asingesubiri kuwezeshwa/kulipwa ili kuutangaza.

..na viongozi wa ccm anaowaomba wamuwezeshe kutangaza ujamaa wenyewe ni makabaila na mabepari uchwara.
Teh teh mjamaa anatembelea vietiiii
Huyu haujuwi ujamaaa
China wenye wanasema wajamaa lkn wanaishi
Kibepari

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Pumba tupu....[emoji706][emoji706][emoji706][emoji706][emoji706]
 
Nakushukuru kwa muhutasari huu, ni bahati mbaya vijana wetu hawana uwezo wa kuyasoma haya na kuyaelewa! Uwezo wao unaishia - "ANACHUKUA ANA WEKA WAAA!" Utajua akili zao ziko hivyo kufuatana na watakavyo changia hapa - subiri!
Inasikitisha sana
 
Nakushukuru kwa muhutasari huu, ni bahati mbaya vijana wetu hawana uwezo wa kuyasoma haya na kuyaelewa! Uwezo wao unaishia - "ANACHUKUA ANA WEKA WAAA!" Utajua akili zao ziko hivyo kufuatana na watakavyo changia hapa - subiri!
Mimi ni mjamaa nasema maghufuli hapanaaaaaaaa tena hapanaaaaaaa sio mjamaa wala ccm hata ujamaa haufahamu ni nini.
 

ujamaa ni umasikini! Unafikiri kwanini USSR ilishidwa na kwanini Nyerere aliondoka na kuacha nchi kwenye majalala.
Kwanini hizi website haziko kwenye nchi za kijamaa, kwanini hatutumii WhatApp ya China!. Kwanini hatutumii soda za china au urusi, kwanini sofware za kazini ni kampuni za mabeberu. Jiulize yote haya kabla ya ku support system ambayo huielewi! China mpaka idadi ya watoto inapangwa na serikali maana yake serikali inatoa mimba kwa lazima ukizidisha!. Kabila ambalo la waislam wapo jela china zaidi ya watu milioni bila kosa. Dini haziruhusiwi wanaabudu Serikali hii ndiyo unataka tuwenayo. China imeanza kuwa tajiri pale ilipoanza kueuhusu makampuni binafsi.
 
Unaomba kazi badala ya kujiajiri. CV ya nini hapa😂😂 elimu bila ujuzi
 
Kwa huu ubunge wa "FINANCE AND BUILDING" tunakupa uwezo huo Tangaza kuanzia sasa [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Huyu bila shaka anaelekea kuchanganyikiwa katika harakati za kujikomba. Mbona CCM wenyewe waliukimbia ujamaa siku nyingi sana baada ya Nyerere kung’atuka? Unawaomba ridhaa ya kupromote ujamaa leo hii?

Awamu ya pili waliweka kikao Zanzibar wakapangua vipengele muhimu vya itikadi ya ujamaa toka Azimio la Arusha na kuunda Azimio la Zanzibar. Tokea wakati huo viongozi wa chama na serikali wakaungana na mabepari wa ndani na nje kujichotea rasilimali za umma kwa maslahi binafsi.

Unatarajia CCM ya JPM iwe tofauti? Hakuna mwenye akili timamu na asiye mnafiki anaweza kushabikia ujamaa. Tatizo letu kubwa leo hii ni jinsi ya kuondokana na mfumo wa ufisadi wa dola (KLEPTOCRACY) na ufujaji unaoendelea chini ya CCM.
 
Napata hasira sana kusikia mijitu kama Deo Sanga mbunge wa Makambako amasema eti "Atake asitake lasima aongezewemuda". Ningekuwa mpiga kura wake ningemchoma sindano ya sumu afe
Deo Sanga alitakiwa kutundulisiwa
 
Wakati wa kuanzisha vijiji vya Ujamaa kuna walichukuliwa Iringa wakapelekwa Arusha,kuna walichukuliwa Morogoro wakapelekwa Songea,kuna watu walichukuliwa Tanga wakapelekwa Mtwara,

Kuna watu wavivu walikuwa wanakasirika walipokuwa wanaamshwa alfajiri kwenda kwenye mashamba ya Ujamaa na kulimishwa.

Lakini kuna Siku Mwalimu Julius Nyerere alitembelea shamba moja Mkoani Tabora alivyofika akapanda juu ya Landrover lakini hakuweza kuona mwisho wa shamba lile la mahindi,Alifurahi sana akatania wasaidizi wake "Sasa natamani kwenda kupumzika Paris,Ufaransa" maana mavuno ya shamba lile yangetosheleza nchi na kubaki na kuuza nchi za nje.

Sasa hapo mwanzo waliokuwa wanakasirika asubuhi na kujiona wapo jela kwenye nchi yao kwa sababu ya kulimishwa,wakati wa mavuno waliimba na kucheza mdundiko na sherehe za kutoa mwali na kuoa zilifanyika maana chakula kilikuwepo,lakini si sasa ambapo wazungu wa haki za binadamu walipoamua kupigavita mifumo hii kuiacha kwa kuwa eti watu walikasirika kuamshwa asubuhi,

Suala sio kuelimishwa,suala ni tabia ya utii na Uzalendo kwa nchi yako,Leo hii nchi kama Korea,China,Cuba,Urusi
bado zipo imara kwenye mifumo hii kwa sababu wameweka mbele Uzalendo na maslahi mapana ya nchi yao,wanajua adui yao mkubwa ni bepari na wamejivisha Uzalendo kwa nchi yao,chochote wafanyacho hata Serikali ikichukua wanaiachia maana cha Serikali ni cha kwao pia,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…