CCM nipe uwezo nitangaze Ujamaa Tanzania kote

Kitako cha Azimio la Arusha kilikuwa kwenye Uongozi bora,Azimio la Arusha liliweka misingi imara ambayo mtu alitakiwa aikamilishe sawa sawa ili akubalike kama kiongozi,

Misingi ya Azimio la Arusha ilikuwa na lengo la kuhakikisha kuwa kiongozi anasimamia ufanisi wa yale yote yaliyotajwa kwenye Azimio la Arusha,asitumie madaraka yake kama namna ya kujipatia au kujiongezea utajiri,

Misingi hiyo iliunganishwa na msingi unaopinga dhuluma kwenye jamii ikiwa inajumuisha aina zote za rushwa.
 
Ujamaaa wakandamize watu lakini wewe ishi kibepari

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Ujamaa ni mfumo wa uongo sana na uliojaa unafiki na ghiliba nyingi kupitiliza! na ulioshtukiwa mapema sana na waasisi wake! Kuanzi Urusi/USSR, China, nk.

Ni mwanadamu mwenye mtindio wa akili pekee ndiye anaweza kuamini ya kwamba UJAMAA UNAISHI! Huu ni mfumo unao wanufaisha zaidi wasimamizi/viongozi wa huo UJAMAA!! Huku kundi kubwa la wananchi mfano Wakulima na Wafanyakazi wakiishi kwenye lindi kubwa la umaskini.
 
Ujamaa ulimshinda Nyerere utauweza wewe. Ujamaa mwisho chumbe. sisi tuliukataa day one. Munatafuta KULA.
 
Ujamaa ulishindwa sababu haukuruhusu natural competition. Yes binadamu wote ni sawa ila kila mtu ana kipaji cha aina yake.
Kutengeneza jamii Yenye kujari uhuru sawa wa kila mtu,na haki ni muhimu sana. Ila kutuweka watu kwenye mafungu ni dhambi kubwa.
Nchi nyingi za kijamaa zilianguka sababu aliyekuwa kwenye nafasi na madaraka, hata kama hafai, alichukuliwa kama ni mtu mkubwa sana. Wakajazana wapiga majungu kwenye nafasi nyeti na kusahau watendaji wenye nia ya kuwatumikia wananchi.
Ilikuwa ni balaa. Tunapoanza kuutangaza tena ujamaa, tuwe tayari kufanya self criticism. Tusije kutengeneza miungu watu. Miungu watu ndio sababu ya kuanguka kwa ujamaa duniani
 

Ulitengeneza Miungu watu ambao walikuwa hawaambiliki. Wapiga majungu. Waliokuwa na uwezo mdogo wa kutenda na waroho wa madaraka.
Walitugawanya kwenye makundi
 
Acha kujikomba mzee,fanya kazi
Nenda kalime etc msipende kuishi
Kwa kupiga domo

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Toa neno kitako weka neno msingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…