Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
CCM njia panda mjadala wa Katiba Wednesday, 29 December 2010 20:50
Hussein Issa
WAKATI joto la madai ya katiba mpya likizidi kupanda, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kinaweza kuitisha kikao maalumu kwa ajili ya kujadili suala hilo kama kitaona kuna umuhimu wa kufanya hivyo.
Katibu Mkuu wa CCM Yussuf Makamba aliliambia gazeti hili jana kuwa kwa mazingira ya sasa, CCM haijaona haja ya kuzungumzia suala hilo kwani misimamo ya serikali ni ya CCM, lakini kama kuna haja kamati Kuu ya Chama hicho itaketi kulizungumzia.
"Mimi kama Makamba siwezi kusema lolote ila Kamati Kuu ya CCM ndio pekee inayoweza kukaa na kujadili mapungufu yaliyopo katika katiba na kutoa ushauri kwa serikali,''alisema na kuongeza: "Lakini Serikali ni CCM na CCM ndio Serikali, hivyo kukiwa na lolote, lazima chama kijadili kwanza kiundani na baadaye kupeleka mapendekezo serikalini kwa ajili ya utekelezaji.
" Makamba alitoa kauli hiyo kujibu hoja la Mdhamini wa CCM, Peter Kisumo ambaye alitaka CCM itolee kauli suala hilo na isiogope kuongoza mjadala wa katiba kwani suala hilo sasa limeshakuwa la jamii.
"Tunaheshimu mawazo ya mzee wetu Kisumo kwani ikilazimika CCM tutakaa na kujadili hili suala kiundani na kama vipi ndugu yangu tutatoa tamko kama tulivyoshauriwa "alisema Makamba. Juzi mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kisumo, alikitaka chama hicho kutoa tamko linaloonyesha msimamo wake kuhusu mjadala huo.
Kisumo alisema CCM haipaswi kuogopa kuongoza mchakato wa mabadiliko ya Katiba kwa kuwa mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa yaliyotokea nchini tangu mwaka 1977, yanalazimisha kuwapo kwa Katiba mpya.
Kisumo, aliitahadharisha CCM na kuitaka iitazame vizuri agenda ya mabadiliko ya Katiba vinginevyo itaonekana ni agenda ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kukipa umaarufu wa bure chama hicho.
Tusiogope suala la kuleta mabadiliko ya Katiba na mimi naitahadharisha CCM kama haitakuwa msitari wa mbele kuongoza agenda hii basi itaonekana ni agenda ya Chadema kama ilivyotokea katika suala la vita ya ufisadi,alisema Kisumo.
Mwanasiasa huyo ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa mabadiliko ya Katiba mwaka 1977, alifafanua kuwa mabadiliko ya katiba ya mwaka 1977 yalisukumwa na kuungana kwa vyama vya TANU na Afro Shiraz Party (ASP).