Pre GE2025 CCM Njombe yawaonya watakaotoa zawadi bila vikao halali

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1735753616427.png

Chama Cha mapinduzi CCM mkoa wa Njombe kimepiga marufuku wanachama wa chama hicho kujipitisha na kutoa zawadi,misaada au kitu chochote katika kipindi hiki bila kuridhiwa na vikao halali vya chama na kwamba hatua Kali za kinidhamu zitachukuliwa kwa atakayebainika.

Kupitia maazimio ya Kikao Cha Halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Njombe katibu wa siasa uenezi na mafunzo Josaya Luoga amesema kwa Mwaka huu wa 2025 hakuna atakayejipitisha na kutoa msaada au zawadi yoyote kwa wananchi au wapiga kura na kuachwa salama kwani hizo ni hujuma dhidi ya waliopo mamlakani katika kata na Majimbo.

Pia soma: Kuelekea 2025 - Mary Chatanda awaonya Madiwani na Wabunge wanaojipitisha kwa Wajumbe ili waungwe mkono

Aidha Luoga amesema Chama hicho kimepiga marufuku tabia za baadhi ya vijana kujirekodi au kutumia vyombo vya habari kuwakaribisha wagombea kwenye kata au Majimbo ili hali muda wa Uchaguzi bado kwani ni kukiuka kanuni za Chama.

Amesema Kuna tabia za baadhi ya vijana kuanza kukaribisha wagombea ili hali Bado Kuna madiwani na wabunge wanaoendelea kufanyakazi Hadi hapo watakapomaliza muda wao.

Hata hivyo Chama Cha mapinduzi CCM mkoa wa Njombe kimewatakia kila lenye heri wanachama na wananchi wote katika Mwaka mpya wa 2025 huku kikiwataka kudumisha amani na kushiriki katika uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura katika zoezi linalotarajia kuanza Januari 12 Hadi 18 Mwaka huu.
 
Tusikilize Live Kupitia 89.1Mhz Na App Ya Radio Box Kama Uko Nje Ya Mkoa Wa Njombe.
Zawadi bila vikao halali,je vipi wanaopatikana bila kura halali,nawa himiza wana mboga mboga wa hapo wajue kuwa hamna haki duniani,haki haiombwi ila inatafutwa tena kweli kweli,huyo sasa ni wakumhakikishia kuwa zawadi ni zawadi tu na ni halali na sii rushwa kupata uongozi,udiwani,ubunge, hata ule mkuu.
 
Chama Cha mapinduzi CCM mkoa wa Njombe kimepiga marufuku wanachama wa chama hicho kujipitisha na kutoa zawadi,misaada au kitu chochote katika kipindi hiki bila kuridhiwa na vikao halali vya chama na kwamba hatua Kali za kinidhamu zitachukuliwa kwa atakayebainika.

Kupitia maazimio ya Kikao Cha Halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Njombe katibu wa siasa uenezi na mafunzo Josaya Luoga amesema kwa Mwaka huu wa 2025 hakuna atakayejipitisha na kutoa msaada au zawadi yoyote kwa wananchi au wapiga kura na kuachwa salama kwani hizo ni hujuma dhidi ya waliopo mamlakani katika kata na Majimbo.

Aidha Luoga amesema Chama hicho kimepiga marufuku tabia za baadhi ya vijana kujirekodi au kutumia vyombo vya habari kuwakaribisha wagombea kwenye kata au Majimbo ili hali muda wa Uchaguzi bado kwani ni kukiuka kanuni za Chama.

Amesema Kuna tabia za baadhi ya vijana kuanza kukaribisha wagombea ili hali Bado Kuna madiwani na wabunge wanaoendelea kufanyakazi Hadi hapo watakapomaliza muda wao.

Hata hivyo Chama Cha mapinduzi CCM mkoa wa Njombe kimewatakia kila lenye heri wanachama na wananchi wote katika Mwaka mpya wa 2025 huku kikiwataka kudumisha amani na kushiriki katika uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura katika zoezi linalotarajia kuanza Januari 12 Hadi 18 Mwaka huu.

Tusikilize Live Kupitia 89.1Mhz Na App Ya Radio Box Kama Uko Nje Ya Mkoa Wa Njombe.
Je jirani zao wenye hizo rangi za bango wanasemaje
 
Wamuonye na Mama yao maana ndio anaongoza kwa kutoa rushwa/takrima!.
 
Back
Top Bottom