Uchaguzi 2020 CCM, Polisi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi acheni kampeni ziendelee

Uchaguzi 2020 CCM, Polisi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi acheni kampeni ziendelee

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2012
Posts
602
Reaction score
2,506
*HUKUMU YA TUME DHIDI YA TUNDU LISSU*

Ukisoma taarifa ya Tume kuhusu Kumsimamisha Tundu Lissu kufanya kampeni SIKU SABA (7) na ukitafakari kwa kina kuhusu Mwenendo na Kanuni za Utoaji Haki;

Unajiuliza kama kweli Tume ya Uchaguzi na Kamati hiyo ya Maadili, ina Wasomi wa Sheria ndani yake.

Kanuni iko hivi;

Kabla hujampa Mlalamikiwa nafasi ya kujitetea, ni lazima upime uzito wa Tuhuma dhidi yake, na Uzito kisheria na kikanuni; kama zinagusa sheria na kudhihirisha uvunjifu wa sheria au kanuni.

Hii ni hatua inayoitwa *Establishment of a Prima Facie Case* na inatakiwa iwe na uzito wa kugusa sheria kiasi cha kumtia hatiani mlalamikiwa iwapo hakupewa nafasi ya kujitetea.

Ni kwa sababu, mtu hatiwi hatiani na kupewa hukumu kwa sababu ya udhaifu wa utetezi wake, bali kwa sababu Mlalamikaji/Mshtaki amethibitisha kiwango cha uvunjifu wa sheria husika.

Kwa hukumu hii; Kamati hii ya Maadili inataka tuamini yafuatayo;

1. Wasimamizi wa Uchaguzi nchi nzima pamoja na Rais; wameitwa kuhojiwa na kutoa ushahidi mbele ya Kamati hiyo, wamethibitisha kila mmoja kwa vielelezo kwamba tarehe iliyotajwa kwamba walikutana kupanga namna ya kuhujumu uchaguzi, kwamba haikuwa hivyo.

Yaani Wakurugenzi wote wameonyesha kwa namna ya kuaminika, kwamba hawakuwepo Dodoma kukutana na Rais. Kila mmoja ameonyesha vielelezo alikokuwa siku husika.

Kwa kufanya hivyo wameishawishi Tume/Kamati kwamba Lissu amewazushia tu.

Swali ni je, Waliolalamika; CCM na chama NRA wamefanya hivyo? Wamemleta Magufuli na kuwaleta Wasimamizi wa Uchaguzi kuzikana tuhuma hizo kwa ushahidi ili Tume/Kamati ilijiridhishe na Uzito wa kesi dhidi ya Lissu kwamba ametunga maneno?

2. Kamati imeletewa nukuu za Maneno ya Uchochezi na ya Kudhalilisha kinyume na Maadili ya Uchaguzi.

Kwamba CCM na NRA wamepeleka mbele ya Kamati hiyo Ushahidi wa Sauti au Video ya Lissu akitoa maneno hayo ambayo Kamati imeyapima dhidi ya Maadili ya Uchaguzi na kujiridhisha kwamba Lissu amekiuka na kuyavunja.

[emoji1614]Ni bahati mbaya Taarifa hii ya Tume ya Uchaguzi haijataja maneno halisi wala haijaweka NUKUU ya Maneno halisi ya Lissu ambayo ametuhumiwa kwayo kwamba yamevunja maadili ya uchaguzi.

Ni maneno yapi hayo?

Wasomaji wa Taarifa hii tumevishwa gunia usoni na kusogezwa Gizani; hatujui maneno hayo ni yapi ili nasi tujiridhishe kwa kusoma maadili hayo tuone na kupima kiwango cha haki iliyotarajiwa kutendeka.

Ni kanuni kwamba *Haki sio tu itendeke, bali pia ionekane ikitendeka.*

Neno *"Maneno ya Kichochezi na ya Kudhalilisha"* sio tu ni tungo TATA bali pia ni Tungo PANA sana _(It's ambiguous and vague term)._

Lissu akiwa majukwaani Mkoani Mara na kwingineko, ameongea maneno mengi sana katika hatuba zake.

Ni vyema Tume na Kamati hiyo ingeeleza "specifically" ni maneno yapi kati ya mengi aliyoongea Mhe. Tundu Lissu, ni ya kichochezi na yanadhalilisha?

Lakini pia ielezwe bayana, maneno hayo yanadhalilisha nani?

[emoji1614] Kama Tume na Kamati ya Maadili ya uchaguzi haikufanya na kuendesha Malalamiko hayo kwa misingi ya mambo haya niliyoeleza; maana yake ni kwamba imemhukumu Mhe. Tundu Lissu bila Upande wa Mashtaka/Mlalamikaji kujenga Kesi yake dhidi ya Lissu.

*Kwa mantiki hiyo, Kamati imefanya kazi yake chini ya Viwango vinavyopaswa kufikiwa na Taasisi za Utoaji haki.*

*Na kwa mazingira hayo, Kamati hiyo imemhukumu Lissu kwa kukosa kujitetea, na sio kwa sababu kesi dhidi yake imethibitishwa kwa viwango vinavyopaswa kisheria.*

Sitaki kuamini kwamba Kamati ya Maadili ya NEC, eti haina Wanasheria, ambao wanajua viwango na taratibu na kanuni za utaoji haki.

Kama ndivyo, basi haya ni makusudi na mwendelezo wa nia ovu na Chuki ambayo Tume kupitia Mkurugenzi wake wameonyesha waziwazi dhidi ya Mhe. Lissu.

Na kwamba adhabu hii na hukumu hii imesimama kwa niaba ya *mabomu* ambayo Dr. Mahera- Mkurugenzi wa Tume aliahidi kuanza kuyatumia kwa kupitia Jeshi la Polisi.

Hilo ni jaribu, hilo nalo litapita.
 
Mgombea urais Tundu Lissu atasimama kufanya kampeni kwa siku 7 ila Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu ataendelea na kampeni za kuwanadi wabunge na madiwani wa Chadema.

Hakuna wa kumstopisha Lissu.
 
Wana jarbu kumpunguzia speed aendane na jiwe lao

SUBIRI KIDOGO
 
Ninavyomjua Lissu atarudi kivingine na atawavuruga wakose kuelewana.
 
Hatukubali uonevu wenu NEC tena sasa mmekuwa adui wa watanzania.
 
Mgombea urais Tundu Lissu atasimama kufanya kampeni kwa siku 7 ila Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu ataendelea na kampeni za kuwanadi wabunge na madiwani wa Chadema.

Hakuna wa kumstopisha Lissu.
Hahahahaaa! Baada ya kuona comment hii nikakumbuka wale waliokua wanatetea kuwa waziri mkuu anafanya kampeni kama mjumbe wa halmashauri kuu na si kama waziri mkuu, swali likawa unawatofautisha saa ngapi, muda gani anakuwa waziri mkuu muda gani anakua mjumbe wa halmashauri kuu, jibu halikupatikana sasa naona what goes around comes around, soon tutamuona makamu mwenyekiti akipambania wagombea wa chama chake wakati mgombe urais atakua amepumzika.

Hila mbaya sana na hazijawahi kushinda siku zote, yaani kama kwelu wangekua wanasimamia haki kama wanavyojinadi, mambo yangekua mapesi sana.

Sent from my itel P13 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom