Malafyale
Platinum Member
- Aug 11, 2008
- 13,833
- 11,173
Gazeti la habari leoiImeandikwa na Ikunda Erick, Dodoma; Tarehe: 9th July 2010
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Dodoma kwa kushirikiana na Polisi wanawahamisha wapangaji kwa nguvu kwenye nyumba za kulala wageni, kwa walichokiita ni kupisha wajumbe na Mkutano Mkuu wa chama hicho.
Tafrani hiyo imeanza leo katika baadhi ya nyumba za kulala wageni , mwandishi wa habari hizi ameshuhudia vitendo hivyo.
Katika nyumba ya Dallas, HABARILEO ilishuhudia wapangaji waliokuwa hapo kwa takribani wiki moja, wakirudishiwa fedha zao za pango kwa siku zilizosalia na kutakiwa kuondoka.
Tumekaa kwa wiki na nusu hivi, na tulikuwa tukae hadi Bunge livunjwe, lakini leo tumefukuzwa, viongozi wa CCM wamekuja na polisi na kutaka wapangaji tuondoke, alisema mmoja wao.
Mwandishi wa habari wa StarTv, Tom Chilala, ni miongoni mwa waliokumbwa na hatua hiyo, na alisema yeye na wenzake walikuwa wanatafuta mahali pengine.
Sekeseke hilo pia liliwakumba wapangaji kwenye nyumba ya Capricorn ambapo wateja waliokuwa wamepanga takriban wiki au zaidi nao walitimuliwa.
Hata hivyo, baadhi ya wapangaji waligoma kuondoka kwenye nyumba hiyo, huku wakichukua funguo za vyumba vyaona kuondoka nazo.
Baadhi ya wapangaji walioondoka na funguo walisema hawawezi kuondoka kwani nao ni binadamu na wanalipa fedha.
Hata hivyo, inasemekana mameneja wa nyumba hizo ambao walionesha kusita kuwatoa wapangaji, walipewa vitisho na baadhi yao kuwekwa rumande, kama njia ya kuwatisha.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili ulibaini kwamba baadhi ya nyumba za kulala ziliandikiwa barua na CCM kuwataarifu kuhusu kuwekewa nafasi.
Kwenye nyumba ya Kilamia, wahudumu walisema hawakusaini mkataba na CCM, ila juzi walifika usiku wakitakavyumba vya watu tisa.
Sisi tuliwaambia vyumba vimejaa, nao wakasema ni lazima wapangaji waondoke, ila tuliwagomea tukawaambia wapangaji wapo hadi Bunge livunjwe, hatuwezi kuwatoa, alisema mmoja wa wahudumu.
Aliongeza alipowajibu hivyo waliondoka na kusema watarudi jioni na polisi kuwatoa kwa nguvu, kwa maana wanachama wa CCM wamekuja kwenye mkutano wa chama, hivyo wanahitaji malazi.
Wingi wa watu unatokana na Mkutano Mkuu wa chama hicho unaofanyika leo na kesho.
Mkutano huo una takribani wajumbe zaidi ya 2,000 kutoka mikoa yote nchini.
My take;Habari hii imenisikitisha sana,sikujua kuwa TZ tumefikia hatua hii ya uvunjaji wa haki za binadamu;mungu tuhurumie!