CCM ruksa kukutana, Wapinzani mwiko kukutana; Tunalibomoa Taifa

CCM ruksa kukutana, Wapinzani mwiko kukutana; Tunalibomoa Taifa

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
539
Reaction score
3,507
Wapo watu wanaona wao ndio walizaliwa kuzungumza,kutafakari sahihi na kuamua kwa ajili ya wengine. Wapo watu wameaminishwa kwamba wanaishi hapa Duniani kupumbuza wengine ili wao na familia zao warithishane madara. Zipo familia Leo baba,mama,watoto wanatumia usafiri wa serikali,wanalipiwa nyumba na serikali, wanalipwa posho kwa kifupi zipo familia kwa mwezi zinagharamiwa zaidi ya milioni 50 Hadi 100 na serikali. Si kwamba wana akili au Wana miujiza ila wameamua kututawala na wanatamani familia zao wazidi kututawala.

Familia hizi zilianza miaka 30 nyuma kukabidhiwa nafasi wakaweka ndugu zao. Wamejiwekea utaratibu kwamba wao wataamua hatma yetu Kama Taifa huku wakiamini kuelimika kwetu ndio ukombozi wetu.

Leo hii wamekuwa na kiburi kufikia kutuamulia Ni Nani tumsikilize na Nani tusimsikilize. CCM Leo hii wameamua kutokupambana kwa hoja Bali kupambana kwa kutumia dola. Kama hoja zinajibiwa kwa dola, Ni lini hoja kinzani zitapata majibu. Polisi hawajibu hoja wanazima hoja, CCM wote kwa ujumla nao wameamua kuishi si kuwapambana kwa hoja Bali kwa kuwatuma polisi wakawanyamazishe watoe hoja. Hi si Hali nzuri na tusipoangalia tunatengeneza kizazi Cha kudai haki ambacho kinaweza kuibukia popote na kuyumbisha amani.
 
Mnasema kuna korona imejaa kila kona alafu hapo hapo mnaanda viukumbi ili mrundikane kama sisimizi!..

Acheni ujinga jamani
 
Mnasema kuna korona imejaa kila kona alafu hapo hapo mnaanda viukumbi ili mrundikane kama sisimizi!..

Acheni ujinga jamani
Hata wewe acha ujinga.
Hakuna tamko lakuzuia shughuli za mikusanyiko kwa sababu ya korona.
Mwenge
Kampeni
Nk vinaendelea
Usawa uwepo kotekote,usiombee kuivunja amani kwa nguvu zisizo za kisheria
 
Back
Top Bottom