Wanachama wa ccm mkoani Rukwa wamekwenda kinyume na msimamo wa chama chao na kutaka uwepo wa serikali tatu maana katiba ni kwa maslahi ya Taifa na sio wana ccm, Tunajua ccm viongozi wakubwa wanataka serikali mbili kwa maslahi yao na sio taifa, wakisahau kuwa kuna uwezekano watoto wao wakaja kuteswa na katiba hiyo hiyo ambayo tutaiwekea ubovu. Tunasikitika na chama chetu maana kinasimamia mambo mengi yaliyotutesa yaendelee kuwepo kwenye katiba hii mpya. Kwa hapo hatuwezi kukubaliana kabisa maana ni muda na sisi kuwa na serikali yetu ya Tanganyika ili tushugulikie changamoto zetu, kusema serikali tatu ni gharama siyo kweli maana ufisadi tu kwa sasa kwa mwaka ni bajeti ya miaka 3. Waliyasema hayo katika mkutano wao katika kijiji cha Kasanga wilaya ya sumbawanga vijijini
nawasilisha
nawasilisha