CCM RUKWA: Tunataka serikali tatu

DOMA

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2011
Posts
944
Reaction score
366
Wanachama wa ccm mkoani Rukwa wamekwenda kinyume na msimamo wa chama chao na kutaka uwepo wa serikali tatu maana katiba ni kwa maslahi ya Taifa na sio wana ccm, Tunajua ccm viongozi wakubwa wanataka serikali mbili kwa maslahi yao na sio taifa, wakisahau kuwa kuna uwezekano watoto wao wakaja kuteswa na katiba hiyo hiyo ambayo tutaiwekea ubovu. Tunasikitika na chama chetu maana kinasimamia mambo mengi yaliyotutesa yaendelee kuwepo kwenye katiba hii mpya. Kwa hapo hatuwezi kukubaliana kabisa maana ni muda na sisi kuwa na serikali yetu ya Tanganyika ili tushugulikie changamoto zetu, kusema serikali tatu ni gharama siyo kweli maana ufisadi tu kwa sasa kwa mwaka ni bajeti ya miaka 3. Waliyasema hayo katika mkutano wao katika kijiji cha Kasanga wilaya ya sumbawanga vijijini
nawasilisha
 
...hawa madogo wanachezea ma------ ya nepi,ngoja aje. Hongereni,msiishie hapo pigeni chini na mbunge wenu maana anaunga mkono hoja msizozitaka...
 
Nape na genge lake watasema ni wana Chadema wana badilisha story hapa .Kazi kubwa hata Rukwa wameamka baada ya kurogwa sana ? CCM mna kazi kubwa
 
Haya ndiyo maoni ya wananchi wanaoipenda nchi yao!
 
Kama wametoa maoni hayo ni sawa. Lakini mi nafikiri serikali moja ingekuwa poa. Mikoa ya zanzibar inabaki kama ilivyo ila tunakuwa na serikali moja tu ya JMT
 
hayo ndo maoni yao lazima tuyaheshimu. kama vile tunayovyoyaheshimu mawazo ya nape ya kutaka tunu za taifa eti zitungiwe sheria badala ya kuwekwa kwenye katiba km sheria mama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…