Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma kimewataka wanachama wake kuhakikisha wanazingatia taratibu, Sheria, na kanuni za Uchaguzi wakati wa mchakato wa uteuzi wa wagombea wa Ubunge na Udiwani. Lengo ni kuwarudisha madarakani wagombea wanaopendwa na wananchi, lakini kwa kufuata miongozo ya chama na siyo kwa njia ya kupitisha wagombea bila ushindani.
Hayo yamebainishwa na Katibu wa CCM mkoa wa Ruvuma, Mohammed Ally Khalifan, akiwa katika ziara yake ya Siku Nne aliyoanza jana katika jimbo la Mbinga Mjini Katika ziara hiyo, amekutana na wanachama wa CCM katika kata za Kikolo, Kihungu, na Kitanda, ambapo ameweza kuzungumza nao sambamba na kuwapatia mafunzo ya Uchaguzi.