CCM, Serikali Mbili ni Bomu Linalosuburi Kuripuka!

CCM, Serikali Mbili ni Bomu Linalosuburi Kuripuka!

reandle

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2009
Posts
11,166
Reaction score
8,148
Kwa bahati mbaya suala la muungano halijapata kuwa the topic of my interest…sifahamu ni kwanini ingawaje kama ningeulizwa bila shaka jibu langu lingekuwa kwamba nchi hii ina matatizo makubwa na ya msingi kabisa pengine kuliko hili la muungano. Na katika hali iliyonisisimua nimekuta kwamba kumbe hata kwenye mchakato wa katiba unaoendelea hivi sasa, suala la muundo wa muungano limekuwa ndo suala kubwa kabisa kiasi cha kuonekana kero kubwa ambayo ilikuwamo kwenye katiba iliyopo ni muundo wa muungano! Haidhuru, Waswahili wanasema "Wengi wape!"

Awali ya yote tujikumbushe kidogo historia ya miaka michache tu iliyopita; pungufu ya robo karne nyuma.

Ndani ya muda huo kulikuwa na dola kubwa kabisa duniani ambalo lilimeza sehemu kubwa ya Bara la Asia na Ulaya kisha likaunda kile ambacho kilifahamika kama The Union of Soviet Socialist Republics, USSR maarufu kama SOVIET! Dola hili lilidumu takribani miongo saba (miaka 70) lakini wakati ukafika dola likaja kumeguka vipande vipande na kupoteza kabisa ile hadhi ya kuitwa USSR! Wakati dola hilo linasambaratika, lilikuwa na watu kiasi cha mara sita ya waliopo Tanzania hivi sasa! Lilikuwa ni dola kubwa kisiasa, kijeshi; and in fact hata kiuchumi!

Likafuata dola lingine, ambalo mashallah; nalo si haba. Hili lilifahamika kama YUGOSLAVIA! Hata kama halikuwa na nguvu kubwa kiuchumi lakini nalo lilikuwa na ushawishi mkubwa sana kwenye siasa za dunia. Dola hili nalo lilidumu kwa miongo saba (miaka 70) na ushee lakini nalo likaja kumeguka vipande vipande na kupotea kabisa kwenye ramani ya dunia! Kuna hili nalo, Czechoslovakia…nako kameshafutika kwenye ramani ya dunia! Mifano ni mingi ikiwa ni pamoja na ya barani Afrika!

Hao wote walipata kuungana hapo kabla na kuwa nchi moja lakini pamoja na kwamba yalikuwa ni madola makubwa kabisa duniani; siku ilipofika yalikuja kuporomoka mithili ya nyumba ya mchanga! Kama hivyo ndivyo, what's so special in TANZANIA?

Ngoja hoja yangu niiongezee vinyama nyama!

CCM wamekuwa wakinadi kuendelea na muundo wa serikali mbili kwenye katiba ijayo. Wamekuwa wakitoa hoja zao za ni namna gani serikali tatu zisivyofaa lakini kwa maoni yangu hoja zao zimekuwa ni dhaifu mno ambazo zinashindwa kuiangalia Tanzania kwa miaka 50 ijayo linapokuja suala la muungano na uncertainties ambazo huendana na Muungano wowote ule duniani. Sina hakika ikiwa CCM wana namna ya kukabiliana na consequences zinazoweza kutokea ikiwa siku moja muungano wetu utakuja kuvunjika. Ni ujinga kudhani kwamba ima faima; muungano wetu wetu hautakuja kuvunjika abadani! What's so special tulichonacho ambacho hao wengine walikosa na ndio maana walikuja kusambaratika?

Katika mfumo wa serikali mbili, itakapotokea muungano umevunjika basi bila shaka Rais wa Muungano atakuwa ameshapoteza uhalali wa kuendelea kuongoza! Tupige mfano CCM wamekula mwereka na CHADEMA wakachukua dola (wakatoa Rais wa Muungano) kisha Wazanzibar ama chini ya CUF au CCM wakashindwa kufanya kazi na CHADEMA na hivyo muungano kusambaratika! Hii maana yake ni kwamba, automatically Rais wa Muungano atakuwa amepoteza sifa za kuongoza hata kama hakupata hata kura moja kutoka Zanzibar! Je, katika hali kama hiyo CCM ambayo itakuwa imeshazikwa kaburini haitafufuka kwa nguvu zote na kudai kuitishwa kwa uchaguzi mpya? Na kwa hakika watakuwa na haki hiyo. Je, CHADEMA nao wanaweza kuwa tayari kuitisha uchaguzi kirahisi rahisi tu wakati Katiba haisemi chochote kuhusu hilo? By the way, katiba ipi wakati Katiba ya Muungano nayo itakuwa imeyoyoma na muungano wake? Na kama CHADEMA (au chama chochote) hawawezi kuwa tayari kuitisha uchaguzi mwingine kirahisi rahisi hivyo; je, CCM iliyokuwa kaburini inaweza kuwa tayari kuachia Golden Opportunity iliyojitokeza huku wakifahamu wazi kwamba Rais aliyepo ameshapoteza uhalali?

Ni kama nauona mgogoro wa madaraka utakaokuja kutatuliwa na Jeshi kuingia viunga vya Magogoni! Hali kama hiyo vile vile itakuwa na nguvu ile ile ikiwa tutaamua kuwa na muungano wa serikali moja.

Lakini wakati nikiiona hali ni tete kupitia serikali mbili au moja, nashawishika kuamini kwamba serikali tatu inaweza kuwa ndiyo suluhusho la Unforeseen Events! Hata kama muungano unavunjika, kwa mara nyingine tena, Rais wa Muungano atakuwa amepoteza uhalali…! Lakini pamoja na kupoteza uhalali, huwezi kusema tena tuitishe uchaguzi kwani aliyepoteza uhalali ni Rais wa Muungano na Muungano haupo tena! Na huwezi kusema kwamba kwavile Muungano umevunjika basi tuitishe uchaguzi mwingine wa kumchagua Rais wa Tanganyika kwani aliyepoteza uhalali ni Rais wa Tanzania na sio wa Tanganyika kwani Tanganyika bado itaendelea kuwapo na alipigiwa kura na Watanganyika tu! Isitoshe, hata Katiba ya Tanganyika itakuwa STILL LEGIT.

Hivyo basi, CCM lazima wafahamu kwamba hawana guarantee ya kuongoza nchi hii miaka yote lakini hata kama wataendelea kuwa madarakani hadi dunia inakwisha bado hata ndani ya uwepo wa CCM bado Muungano unaweza kuvunjika pasi na shaka yoyote! CCM wakilifahamu hili basi pia wanatakiwa kufahamu kwamba serikali mbili au hata moja ni bomu linalsubiri kuripuka.

NAWAKILISHA! JokaKuu, chama, Ritz, EMT, Jasusi, Pasco, Yericko Nyerere




 
Last edited by a moderator:
Mkuu NasDaz
Muungano unatakiwa ni ridhaa ya wananchi sio viongozi; kama tumeamua kuwa na muungano wa dhati sioni hata hiyo sababu ya kuwa na serikali mbili tunatakiwa na serikali moja itakayo watumikia watanzania; Kinachoogopesha kwa hawa ndugu zetu ni choyo na ubinafsi; Zanzibar imebebwa sana hasa baada ya kuanguka kwa zao la karafuu; walipopata fununu ya mafuta kitu cha kwanza walichokimbilia kusema "nishati haimo kwgenye muungano" nilijiuliza hivi ile gesi ya Songosongo sio nishati? Mbona ilipogunduliwa hawakusema haimo kwenye muungano? Almasi; dhahabu; mkonge; pamba; kahawa zote hizo tulitumia kwa pamoja hatukuhoji mambo ya muungano. Umegusia USSR; Russia ilibeba mzigo mkubwa na hata leo kuna baadhi ya nchi zinatamani zirudi tena kwenye USSR; sasa hawa ndugu zetu wanadanganywa na wanasiasa wenye uchu na kiu ya madaraka lakini ni ukweli usikificho wananchi wa kawaida wa Zanzibar wananufaika sana na matunda ya muungano; hivi mnyaturu wa Singida ananufaika kitu gani na muungano huu??? ikibidi kufa na ufe!!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom