CCM si Safi!

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Posts
4,526
Reaction score
1,540
CCM ni chama, kinaongozwa na watu ambao wako Serikalini kama viongoZi wenye mamlaka ambao wanajilimbikizia mali kiujanjaujanja, kuruhusu upotevu wa mali ya umma (CAG report) na ufisadi mwingi tuu.

Hivyo ni sahihi sana kusema CCM imejaa rushwa maana wale walioko ndani ya chama Kama watendaji, ni tegemezi wa viongozi wa chama ambao ni viongozi wa Serikali na hakuna mfumo mzuri wa kukosoana kwa kuhofiana.

CCM si safi, maana kama Lowassa katuhumiwa kwa miaka 20 kujipatia mali na minong'ono kuwa ni fisadi bila kuwa na vikao vya chama kumhoji na hata kumvua uanachama mpaka akadiriki kutaka kugombea Urais kupitia CCM kitu ambacho kingemfanya awe mwenyekiti, hapo ni wazi Chama kina mapungufu makubwa.

Hata katika safu ya ugombea ubunge, zaidi ya nusu ya watakaogombea ubunge wa CCM ni watu wenye kutiliwa mashaka makubwa kimaadili; wananuka rushwa na ufisadi mtupu. Lakini kwa kuwa ni marafiki wa wafanya maamuzi ndani ya chama au tayari wana nafasi za kimadaraka ndani ya chama wanaachwa wendelee na hata kuwa wabunge halafu tunajiuliza ni watu gani wanakwenda Bungeni.

Udhaifu huu wa chama kukosa uongozi imara na makini wenye kuweza kudhibiti utovu wa nidhamu wa wanachama wake hata viongozi ulijionyesha wazi kwa watu 42 waliochukua fomu na kutangaza nia kutaka uraisi huku ikijulikana wazi wengi wao hawana uwezo hata kidogo kuwa Rais au Mwenyekiti wa CCM, wenye ukosefu wa maadili (si ufisadi pekee) na mambo mengine mengi ( hata ubunge wengi wao hawafai, na wameshindwa kazi).

Aidha kitendo cha viongozi wengine waliko kwenye halmashauri kuu, kumshangilia bila woga Lowassa na kuimba wana Imani naye ilikuwa ni kitendo cha dharau kubwa kwa uongozi hasa mwenyekiti, makamu, katibu mkuu na Kamati Kuu.

Yote haya yanaashiria udhaifu wa Chama pamoja na kelele zote za Nape kujifanya kuwa chama ni makini!

Hivyo mawazo na kauli kudai CCM haina matatizo bali ni mtu mmoja mmoja fisadi au mkosa maadili hakuna mantiki wala usahihi!

Ubaya zaidi, CCM inamnadi mtu wa kutetea Status Quo, mchekeshaji kama JK 2005, kulinda maslahi ya wale waliobakia ndani ya chama ambao lengo lao kuu ni maslahi binafsi na si maslahi ya nchi. Watu wenye maadili na umakini wasiotabirika ndani ya chama walikatwa (Pinda, Mwandosya, Jaji Ramadhani, Dr. Bilali) kwa makusudi kabisa hata kufikishwa kamati kuu au NEC kwa kuwa nia si kuleta mabadiliko ndani ya chama kama watangaza nia kadhaa walivyoashiria ndani ya kampeni za kugombea Urais ndani ya CCM (Tanzania Mpya, Tanzania Mabadiliko au VIta vya Rushwa na Ufisadi).

CCM inajukumu kubwa kujibadilisha kabisa na kuunda mfumo makini na imara wa Uwajibikaji na Maadili kuanzia ngazi za chini hadi kitaifa. Na uwajibikaji na maadili, si kwenye ufisadi tuu bali ni katika kila kitu; kuhakikisha haki inatumika, kanuni na sheria zinafuatwa, uzembe, uvivu, uhujumu na utovu wa nidhamu vina kemewa na kuadhibiwa kwa kufuata kanuni na mambo mengine mengi.

Kama CCM ilidiriki kutumia ujanjaujanja na uhuni hata kukiuka miongozo na kanuni katika mchakato wa kumchagua mgombea Urais wake, ni ushahidi gani mwingine tunahitaji kuonyesha kuwa CCM ni tatizo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…