Elections 2010 CCM si shwari tena, maandamano yaanza!

Ex Spy

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2007
Posts
222
Reaction score
1,827


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Juma Simba Gadafi (mwenye baraghashia kichwani) akijaribu kuwatuliza wana CCM kutoka Kata ya Mchikichini Ilala na Miburani Temeke walioandamana leo katika ofisi hizo kutaka kurudisha kadi za chama hicho ama kurudishiwa Wagombea Udiwani waliowachagua wao katika Kata zao.









Picha na maelezo kwa hisani ya blog za Mroki Mroki na Lukwangule
 

Wakisikiliza Kauli ya Gadafi ....


Gadafi alimudu kuwatuliza wanaCCM hao na hapawalikuwa wakimshangilia na kuimba CCM, CCM, CCM na kusubiri hatma ya kilio chao kutoka uongozi wa mkoa.
 
na baada ya mkutano mkuu wa kuwapitisha wabunge na madiwani ndio kitawaka zaid
 
Mwanzo wa ngoma ni lele...

Muda mfupi utajo ngoma hii itanoga sana
 
huu ndio wakati mzuri wa kutafuta mbinu za kupenya ndani ya CCM na kuivunja kabisa, nadhani mara nyingi upinzani huwa unajisahau na unabakia kuwa pembeni kutazama mtafaruku bila kuweka fitna
 
huu ndio wakati mzuri wa kutafuta mbinu za kupenya ndani ya CCM na kuivunja kabisa, nadhani mara nyingi upinzani huwa unajisahau na unabakia kuwa pembeni kutazama mtafaruku bila kuweka fitna
Unajuaje hawako ndani, mimi si mwanaCCM lakini nililetewa kadi nyumbani Jumamosi nikaambiwa kesho yake nikapige kura.
 
Dhana nzima ya poliks za kibongo NI FULL COMEDY..yaani Steven Spielberg anaweza kutengeza muvi kali sana.
 
Unajuaje hawako ndani, mimi si mwanaCCM lakini nililetewa kadi nyumbani Jumamosi nikaambiwa kesho yake nikapige kura.

...Ulikubali au ulikataa wito huo?
 
Tatizo ni zaidi ya tatizo, CCM siku zote haiheshimu demokrasia, and now inadhihirika wanapoendesha mambo yao wenyewe. Ukiangalia kwa makini hao waandamanaji wanasukumwa zaidi na beliefs kwamba mgombea wao ameshinda ........... au ameshiondwa isivyo halali. As such hata ukitengua matokeo ukampa huyo mgombea wao the other side nayo italalamika tu.........

Sasa mzizi wa fitina uko wapi? It is simple demokrasia ya kweli na consistency from top down haipo CCM.
 
CCM ndio yao haya. Wamezoea kuvuruga maamuzi ya watu. Sasa wameibiana wenyewe kwa wenyewe, wanakuwa mbogo. Na subiri uone itakavyokuwa wakati vigogo wao watakapopitishwa kwa nguvu.

CCM ilibadilisha matokeo ya uchaguzi Zanzibar, wakaandamana watu wakala shaba. Sasa sijui wataanza kuwindana au vipi? Maana wanasema DOLA ni yao. Wanaweza kuamuru Polisi wapige risasi waandamaji. Si ndivyo walivyo?
 
...............ngoma ikilia sana mwisho hupasuka!!!!!!!

Hahahahaaaa
 
Dah, Mbeya nako nasikia wanachama wamekasirika sana na kuamua kurudisha kadi za chama huku wakiwa wameandamana kwa mamia... Hii ni ishara mbaya kwa CCM
 
mara nyingi kitu kikioza kwa ndani kwa muda mrefu,matokeo yake huwa ndio haya.......
 
Jipu lazima lipasuliwe! laa sivyo karaha zake haziwezi kwisha pasipo kukitoa kiini..
 
Heri wanaandamana wakipingana wenyewe kwa wenyewe kwenye nchi ya amani na utulivu lakini ole wao Chadema ama CUF waandamane kupinga ushindi wa CCM, hapo amani imevurugika na wanakuwa kama vile wametangaza vita dhidi ya dola - shuhudia vijana wa Mwema watakavyowashukia kwa marungu na mabomu ya machozi ! Duh, nchi hii kweli ina wenyewe !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…