MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,252
- 8,003
CCM tulimpamba mzee sana kuanzia bungeni na nje ya bunge, tukaenda mbali na kusema kuwa hahitaji kampeni 2020 bora hata uchaguzi usifanyike ili apite bila kupingwa, hizi kauli za kinafki ni za kumhujumu mgombea wetu kuanzia leo iwe mwisho. Kama kweli hatukuhitaji kampeni wala uchaguzi huo CHOPA ni ya nini? Gharama zote za Chopa za nini?
Natoa wito kwa wanaccm wote, tuache unafki wa kumpamba mzee wetu wakati tunajua kuwa hali ni ngumu na uwezekano wa kuzidiwa ni mkubwa sana. Tunamdanganya mzee wetu kuwa mambo ni shwari kwa manufaa ya nani? Tukishindwa wa kwanza kupata hasara ni nani kama siyo mimi na wewe?
Kwa bahati mbaya sana chama chetu makao makuu kwenye uongozi timu nzima ya kampeni ni wageni wa siasa za nchi hii, Dr Bashiru na Polepole wameingia kwenye siasa juzi juzi. Hapa ukimtoa mzee Mangula wengine wote waliobaki ni wa kuja watupu na ndio wanaokigharimu chama hawa. Sitaki kuwa mnafki huu ndio ukweli acha niseme tu.
Nipo kwenye timu ya kampeni ndiyo na tunatazamana hapa wacha niseme ukweli mwenye kununa anune, mkiambiwa ukweli mnakua wakali.