CCM Tabora yaamua kuboresha uwanja wa Ali Hassan Mwinyi baada ya kufungiwa na TFF

CCM Tabora yaamua kuboresha uwanja wa Ali Hassan Mwinyi baada ya kufungiwa na TFF

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Siku moja baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, kuufungia uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora, kutumika katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kukosa vigezo na kanuni za mpira wa miguu, wamiliki wa uwanja huo ambao ni Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Tabora wameanza kuufanyia maboresho uwanja huo na kutoa uhakika wa kukamilisha maboresho hayo ndani ya siku kumi na nne ili uanze kutumika tena.

Soma Pia: Baada ya mechi ya Tabora na Yanga kukaribia TFF waufungia Uwanja waAlly Hasani Mwinyi uliokua unatumiwa na Tabora United

 
Shida ya uo uwanja sio nyasi pekee, wanatakiwa watoe uo udongo wa juu wa sehemu ya kuchezea waweke udongo mpya na kupanda nyasi husika.
Ndani ya mwezi na nusu uwanja utakua tayari na utadumu kwa muda mrefu.
Iyo ardhi ya uwanjani ni ngumu na ina mashimo mengi ata mkipanda nyasi na kumwaglia haita saidia kuondoa tatizo.
 
Eti chama cha siasa kinamiliki viwanja vya mpira. Hii nchi tunacheleweshwa sana.
kwamba hufahamu karibu mikoa yote ccm anamiliki viwanja vya michezo

kama hujui hili basi na wewe ni sehemu ya ccm kutumia kutuchelewesha
 
Back
Top Bottom