Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Jana Alahamisi jioni luninga ya Chaneli Ten ilionesha kikundi cha UVCCM wakiwa stesheni ya SGR ya Dar as Salaam tayari kwa kupanda treni kwenda Morogoro na kurudi, kikundi hicho kilipokelewa na meneja mkuu Kadogosa ambaye alionekana akitia maelezo kuhusu reli na treni hiyo.
Hivi vikundi vya wanaccm ambao wamejuwa wakipewa burudani ya kusafiri bure kwenye treni hiyo ni vingi tangu treni ilipoanza majaribio mpaka sasa wakati wa kufanya biashara.
Tutarajie kuwepo na vikundi vingine vya wanaccm vitakavyoanzia Morogoro kwenda Dodoma na baadae vitakavyoanzia Dodoma kwenda Tabora na kutoka Tabora kwenda Mpanda, Tabora kwenda Kigoma na Tabora Mwanza.
TRC na serikali lazima vitambue kuwa reli hii ya SGR ni mali ya serikali si mali ya CCM kwa ajili ya kuwapa burudani ya kusafiri wanachama wake, hasara inayopatikana kwa kusafirisha makundi ya wanaccm bila kulipa nauli itaingizwa kwenye kodi ili watanzania wote bila kujali vyama tuweze kufidia hasara, hii haitakuwa haki kwetu.
CCM mpaka sasa imekwisha hujumu miradi mingi vikiwemo viwanda ambavyo vimefia mikononi mwake bila kuchukua hatua za kuviokoa.
Watanzania tutashuhudia kama mradi wa mabasi UDART unavyokufa ndivyo na SGR itakavyokufa bila ya msaada wa kuwekewa dripu.