CCM tukikubaliana na haya, 2025 tumekwisha na tusahau kabisa kutawala tena

Umeeleweka. Ila "by the natural social forces" hata muyakatae haya hamuwezi kutawala milele. "Suppression has always a deadly end".
 
Ccm wakisikia katiba mpya wanachanganyikiwa wanajua ndo mwisho wao
 
Naona kwa sasa tutapaa kiuchumi. Hapo bado tunatumia za Tozo. Bado za Bandali, Madini N.K
 
Moja kati ya consequences za kupora uchaguzi ndiyo msingi wa watu kudai katiba mpya.

Hili ndilo suruhisho pekeee la kuwaadhibu.

Katika nchi ya kidemokrasia huwezi puuza kura za watu miaka mingi ukaishi.

Leo tume la uchaguzi haliaminiki tena kwani miongozo yote inapindishwa kufuata matakwa ya watawala.

Dhambi hii ndiyo mzizi wa dai la katiba. Tunakoelekea kama tabia hii itashamiri pengine itawatia akili.

Ni ukweli usiopingika sasa watanzania wanataka kura yao iheshimiwe.

Pasiwe na mtu aliye juu ya kura zao!
Ili ukiwapuuza na wao wakupuuze!

Na mimi binafsi ninaungana na mawazo yao.

Katiba mpya itakuwa ni heshima ya kura za watanzania.
Katiba mpya itakuwa ni serikali sikivu kwa watanzania.
Katiba mpya itakuwa ni njia ya kurudisha nidhamu ya viongozi wa kisiasa kwa wananchi, kama Magufuli alivyojinadi kurudisha nidhamu ya watumishi wa umma.

Viongozi wengi wa kuteuliwa na rais hawana nidhamu kwa wananchi bali wananidhamu kwa raisi aliyepa mikate.

Na raisi kwa mamlaka makubwa aliyonayo hata ya kupora uchaguzi na kuwa na uhakika wa kupita bila kura "hata mkipiga kura kwingine, tutaunda serikali" ni vigumu kuwasikiliza na kuguswa na maumivu ya wananchi!

KATIBA MPYA NI SASA, KATIBA MPYA NI HESHIMA YA VIONGOZI KWA WANANCHI
 
Hapo nina wasiwasi, Chadema sindowalikuwa wanalalama kuhusu JPM, sasa hivi ndo wanatamani wasimamishe mtu kama JPM? Sidhani kama ni kweli.
 
Polisisiem na tisissiem wameenda wapi.
 
Usitubugudhi mkuu, sisi hatutegemei wananchi wala 2025 yako, sisi tuna Siro na Tume, vinatutosha mno hivyo. Mengine ni mafomalitizi tu
Siro atakuwa ashastaafu hadi hio 2025 hata kama mmemuahidi ubunge akistaafu bado ccm ngoma ngumu 2025.IGP mpya atafanya kazi professional atokubali jeshi litumike kisiasa.
Kama jiwe na mabavu yake yote na kwa kumtumia Mahera,mtungi, wakurugenzi, police still alikataliwa live hadi akapiga magoti na kugalagala ikiwemo kutishia live kuwanyima maendeleo still alipenya kwa binde.Ccm kwa sasa haina mtu anaeuzika kwa wananchi.2025 lzm ilale,mama ndo auziki kabisa.
Nakwenda kuyaona ya Zambia,Malawi,Ghana na Nigeria yakijitokeza nchini kwetu.
Ya raisi kufia madarakani kisha ashika raisi wa mpito uchaguzi mkuu anapigwa chini na wananchi mpinzani anashinda ndo yaliyotokea nchi hizo.
Ishu ya machinga na ukosefu wa ajira inakwenda kuibamizwa vibaya CCM.
 
Wanaenda kununua mindege 16 kwa zaidi ya trillion 5 waliyolipa kwa cash ambayo kila mwaka inaingiza hasara kubwa kwa Taifa halafu hapo hapo wanasema hawana pesa ya kuajiri madaktari, Wahandisi , Wahasibu, Manesi etc!!!! Akili za wapi hizi!!!?


..tatizo la AJIRA.

..tatizo la GHARAMA ZA MAISHA.

..msiposhughulikia hayo hali ya kisiasa itakuwa tete sana.
 
Mama kumbuka nyongeza ya mishahara 01 May 2021 bado siku 192 tu.KAZI IENDELEEEE
 
Unafiki wako unajitokeza katika aya hii hapa, mengine yote ni mapambio tu.

Mtakuwa na kazi kubwa sana ya kuzuia uwepo wa Katiba mpya, huku mkiwa na matarajio ya kuendelea kuwafanya waTanzania kuwa ni wapumbavu.
 
Wanaenda kununua mindege 16 kwa zaidi ya trillion 5 waliyolipa kwa cash ambayo kila mwaka inaingiza hasara kubwa kwa Taifa halafu hapo hapo wanasema hawana pesa ya kuajiri madaktari, Wahandisi , Wahasibu, Manesi etc!!!! Akili za wapi hizi!!!?
Na hawana habari kabisa na "Wamachinga", ..., akili za tope hizi!
 
Reactions: BAK
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…