CCM tumeiharibu wenyewe, tunabeba wezi, mafisadi, wapiga deal badala ya kuwashtaki na kuwafunga

CCM tumeiharibu wenyewe, tunabeba wezi, mafisadi, wapiga deal badala ya kuwashtaki na kuwafunga

NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2019
Posts
9,863
Reaction score
20,806
Huo ndio ukweli mchungu sana ambao mwanaccm anatakiwa kuukubali.

Ufisadi,wizi,rushwa na upigaji dili Kwa asilimia kubwa wahusika ni wanaccm,Cha kushangaza hakuna hata mmoja yupo korokoroni,wanapeta Tena wanateuliwa nafasi nyingine Ili kuwasafisha.

Chama kinapoteza mvuto,tunatukanwa na upinzani halafu tunatumia Dola kuwatisha badala ya kusafisha chama Kwa kuwafunga wezi,hakuna namna zaidi ya kuwafunga wabadhirifu Ili tusafishe chama hizi propaganda za uchawa hizi hazitosaidia Chama zaidi ya kuwatia hasira wananchi tu!!

Ripoti za CAG zipo wazi lakini hakuna hata mmoja aliewajibishwa,najiuliza huyo CAG tunamlipa mshahara wa nini kama wabadhirifu hawafungwi!!?

Wananchi wanatuchora TU,hatuwezi msafisha mwizi kwa nembo ya chama tukapona kwenye chaguzi zetu,nashauri wezi waanze kufunguliwa mashataka rasmi na kufungwa Ili turudishe Imani kwa wananchi kwamba tupo serious na dola ,lakini Kwa Hali ilivyo hatuwezi toboa bila ujanja ujanja wa kutumia Dola!!

Bado tunao muda was kutosha kufanya hayo kabla ya uchaguzi mkuu!

Yona lazima atoswe baharini Ili kukiponya chama!chama hakijengwi Kwa kuwateua watu wale wale wenye kashfa bali kuwafunga kabisa bila hiyana!

SWALA LA KATIBA NI FIMBO PIA ITAKAYOTUMIKA KUTUPIGIA BADO TUNA MUDA TUFANYE JAMBO MAPEMA ,UJANJA UJANJA HUU WA KUJIBU HOJA KWA VITUKO HAUTUSAIDII,KATIBA MPYA MCHAKATO TULIANZISHA WENYEWE MIAKA KARIBU KUMI,TUMALIZIE TUWAPE WATANZANIA HAKI YAO,TUACHE BLAH BLAH!RASIMU IPO,WANASHERIA TUNAO !MZEE WARIOBA YUPO TUNAKWEPA NINI!!?

Mungu ibariki Tanzania.
 
Muhimu ni CCM iendelee kupoteana mana imetufikisha hapa .
Zumuni la Muungano ilikuwa ni kuimeza Zanzibar yote iwe ndani ya JMT, ndo mana Tanganyika ikasalimisha mambo yake yote ndani ya JMT, lakini Wazanzibar wamegoma kusalimisha mambo yao ndani ya JMT, hapa Kuna haja ya kurudisha serikali ya Tanganyika Ili isimamie mambo ya Watanganyika. Kama SMZ inavyosimamia mambo ya wazanzibar.
 
Back
Top Bottom