MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,252
- 8,003
Kama ambavyo wapinzanzani wetu wamekua wakitupachika kina la Chama cha Majambazi kutokana viashiria vya matendo ya wanaccm wachache waliothaminiwa wakapewa nafasi serikali na chama lakini wanaendekeza tamaa, Wizi, unyang'anyi, utapeli, Ubabe, uonevu na uporaji wa mali za watu. Hii siyo misingi ya Chama cha Mapinduzi aliyotuachia mwalimu Nyerere.
Nachukia na kushangazwa kujitokeza na kushamiri kwa magenge ndani ya Chama ambayo kazi yao ni kutetea wezi, Waporaji wa kutumia silaha, waonevu, Wahujumu uchumi na wabakaji kwa kivuli cha uongozi ndani ya serikali. Hii ni tabia mbaya na ya kukemewa, tusiwape wapinzani wetu kutuita chama cha Majambazi kwa kutetea Maharamia wa aina hii ambao wanaotuchafulia chama na serikali. Ni Upumbavu na uhayawani kutetea Majambazi ndani ya chama na kamwe siwezi kua sehemu ya upuuzi huo.
CCM TUJISAFISHE BADALA YA KUJICHAFUA WENYEWE
Hatua zinazochukuliwa na serikali dhidi ya vitendo viuvo bila kutazama uso wa mtu ndio hatua pekee ya kukisafisha Chama na serikali. Serikali iliyopo madarakani ni ya CCM na siyo ya Chama kiingine.Kwani wapinzani wakifurahia hatua tunazozichukua si ndiyo namna pekee ya kuwaziba midomo wasiongee? Tunataka waendelee kutunyooshea vidole na kutuita chama cha Majambazi?
Nashauri tukae kimya tusitetee magenge ya Wanyang'anyi ndani ya chama na serikali. Rais alishasema tusahau yaliyopita tugange yajayo, sasa ninyi kikundi cha wahuni wachache mnataka kuturudisha tulipofika?
RAIS NA MWENYEKITI WA CHAMA TAIFA CHUKUA HATUA
Nitoe rai kwa Mhe Mwenyekiti wa chama taifa na Rais wa Jamhuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Chukua hatua kwa wote wanaokichafua chama chetu na serikali yetu. Sisi wazalendo wa kweli na wana CCM safi tutaendelea kukutetea na kukuunga mkono. Tumbua majambazi ndani ya chama na serikali, siyo kwa sababu Wewe ni Mama ndiyo maana wanaongea ongea tu, chukua hatua bila kuangalia uso wa mtu na wewe ni mchamungu ulisema serikali yako haitakuwa ya dhuluma.
Nimalizie kwa kusema, iwe mwanzo na mwisho kwamwanaccm kutetea wezi, si hulka na tabia yetu, tuiache serikali ifanye kazi yake kwani ina macho mengi.