Frustration
JF-Expert Member
- Jan 30, 2018
- 3,134
- 4,124
CCM tuna utaratibu wetu wa kumuombea mtu msamaha kisha mkosaji anaenda mbele ya kadamnasi na kutamka maneno machache tu, NI SAMEHE MIMI NIMEKOSA NISAMEHE MIMI NIMEKOSA.
Maneno haya huja baada ya kupitia tanuri la moto na viapo vingi sana mbele ya viongozi wakuu wa CCM. Tena utazungushwa sana hadi kuja kukutana na viongozi wote kwa wakati wao.
Awali utaanza kumtuma mtu aende akakuombee msamaha ila kadri ngoma inavyovuma utaambiwa kamwombe kwanza msamaha mtu fulani, halafu unapoenda tunapiga tu simu mtu fulani anakuja hapo. Aah ukija mara hayupo mara yupo bize mara nenda home kwake nako ukienda njoo kesho ofisini, tena uje kwa maandishi alafu eti ni katibu wa wilaya yako hahahahaha CCM inawenyewe.
Nimeyasema haya ili mjue msamaha ndani ya CCM sio kazi nyepesi, hivyo iwe mtumishi wa serikali au chama muwe makini sana ili msiingie huko. Bila kusahau asante nyingi sana za vitendo kwa kila hatua unayopitia.
BACK TO COMRADE SABAYA
Kuna watu walijaribu kupiga simu oohh asamehewe kwani alikuwa anafanya vile kwa kutekeleza maamrisho ya rais hayati, walivyojibiwa kasimu ni shahidi. Siwezi kusema kuwa anaonewa Sabaya ila kosa lilitengenezwa na awamu ya tano.
Awamu ile ili dump na kudust kila kitu cha awamu ya 4 utazani urais sio taasisi endelevu. Haifahamiki kwa nn hayati alitaka kufanya vile ila huenda dhamira yake ya kuifikisha nchi kwenye uchumi wa viwanda.
Aliamini aliowakuta madarakani wote wezi na ndio waliolitia hasara taifa bila kujua urais ni zaidi ya mechanics work. Akawa taaratibu akifufua watu wapya na kuwaingiza katika mfumo wa nchi na deep state,huku akitupa vijembe kwa waasisi na wafia chama.
Timu mpya aliyoisuka ilikuwa haiendani na Chama,sura mpya kama Sabaya, Makonda etc wakawa wamepewa power zaidi ya waziri, yeyote. Sura hizi ndizo tools za hayati kuibadili nchi kutoka katika mafisadi na wala rushwa waliotopea kwa imani yake.
Kwa kweli baadhi waliimba nae nyimbo moja ila mimi na Kinana ndio watu wa kwanza kukataa kushirikiana nae. Baadae wengine walifuata na wengi wao wakawa kwenye kivuli cha unafiki.
Kuna watu walitumwa kimkakati awe rais wa mihula minne ili kutengeneza Magufuli regime au iundwe Magufuri party kuwa mbadala wa CCM.
Hatimaye haikuwa tena chagua CCM bali chagua Magufuri Hapa Kazi Tu. Slogan hii ilinichefua sana na walienda mbali kudai kila kitu kafanya Magufuli na sio Serikali. Alikiua chama na mwishowe serikali yote ikawa mfukoni mwake na hapo magazeti ya Tanzanite yakawa ndio role mode ya magazeti yote Tanzania.
Kwa hali hiyo sisi kama UVCCM tunashindwa kumsaidia Sabaya kwa sababu hakuwa mwana CCM mtiifu kwa chama bali kwa rais tu. Sabaya alijua CCM na CHDEMA ni fisi na mbwa kumbe hapana bali ni paka na mbwa hatugombani bali tunashindana tu katika chaguzi.
Sabaya anatafuna karma yake na CCM hatuwezi kumuingilia japo hataozea gerezani.