Pre GE2025 CCM tusibweteke na anguko la CHADEMA, bado kuna upinzani wa vyama 14

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Chonde chonde wanaCCM wenzangu. Tusibweteke na anguko la kilichokuwa chama kikuu cha upinzani CHADEMA. Tukumbuke kuna uwezekano wa vyama 14 kuleta upinzani mkali kuliko uliokuwa kwa CHADEMA. Binafsi nakihofia sana UPDP ya kina Fahmi Dovutwa.

Tunachotakiwa kufurahia ni CHADEMA kutusaidia kukibomoa chama chao wenyewe kabla ya uchaguzi mkuu. Vyama 14 haviwezi kufurukuta kwa huu muda uliobaki kabla ya uchaguzi mkuu.

Ninashauri viongozi wa CCM kuweka wagombea ubunge wenye sifa na wanaohitajika na wapiga kura majimboni. Kwenye ubunge huenda kukawa na upinzani kiasi tofauti na nafasi ya Rais ambayo hadi sasa Mbowe kwa kushirikiana na wenzake wameshamsaidia Mama Samia kushinda kilaini.
 
Mwendo ni ule ule hakuna mkate mgumu mbele ya chai😃
 
Eti anguko la Chadema?


Anguko gani? Kinachotokea sio anguko ila Chadema wanawaonesha Watanzania kuwa wao ni chama cha demokrasia kweli maana ushindani unaonekana wazi na wagombea wanachuana vilivyo hadi Watanzania wanaona anayepatikana amestahili
 
Eti Dovutwa mtu ambaye hata walala hoi hawamjui.
 
Eti angulo la Chadema?


Anguko gani? Kinachotokea sio anguko ila Chadema wanawaonesha Watanzania kuwa wao ni chama cha demokrasia kweli maana ushindani unaonekana wazi na wagombea wanachuana vilivyo hadi Watanzania wanaona anayepatikana amestahili
Too late
 
Anguko la CDM au CCM, hahaaaaahaaaaaaaaaaa!
 
CHADEMA ya Leo ni Imara Zaidi ile ya Jana.
 
Najua mumewekeza nguvu nyingi kuibomoa Chadema, Sultan kabadili gia angani, hela yenu b12 kavuta na tarehe 21 anaachia kiti rasmi na cha kumfanya hamna ,cha mlevi huliwa na mgema Sultan kamuingiza chaka maza na Chadema itaenda kuwa bora zaidi.
 
 

Attachments

  • downloadfile-22.jpg
    94.3 KB · Views: 3
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…