Mshangai
JF-Expert Member
- Feb 16, 2008
- 468
- 1,086
Mimi ni mwanaccm asili, sijajiunga Jana au juzi kwa mihemko bali niko hapa kabla hata ya muundo wa vyama vingi.
Ni vizuri kusema ukweli tukielekea uchaguzi mkuu 2020, ile habari ya kutegemea chama chetu kitatumia ujanja na ubabe wa dola tuweke pembeni maana kwa sasa ni hatari kwani tumesha jijengea uadui na jumuia ya kimataifa hivyo madhara yaweza kuwa makubwa.
Nimepita maeneo mengi kuanzia watumishi wa umma wakiwemo polisi na wanajeshi, ukweli wametuchoka sana hata kama wanaimba mapambio kutusifu. Tukumbuke kura ni siri ya mtu.
Wanafunzi na makundi mengine wakiwapo baadhi ya wakulima wa maeneo kadhaa wameshtuka sio wale wa zamani.
Tutaponea wapi? Kukaa na kujidanganya ushirikiano na kina Mbatia au wabunge waliokimbia CHADEMA ambao hawana mvuto ni kujidanganya na kupoteza matumaini.
Ni wakati wa kuacha propaganda za uongo na visa kwa wapinzani, tujikite kurudisha imani kwa wananchi la sivyo uchaguzi wa Oktoba Upinzani hususani Chadema wanaenda kutugaragaza kwa aibu kubwa.
Na kama tutatumia mabavu au wizi wa kura tutegemee viongozi wetu kuishia The Hague kisha jela na chama chetu kusambaratika.
Kwa vijana mihemko wa sasa ndani ya chama chetu wataona hizi ni njozi lakini ndio ukweli maana kifo cha mzee kina mshindo.
Kama viongozi wa sasa wapo ili kukipoteza chama tuwakatae kabisa.