CCM Ujamaa vs CCM Upebari

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,117
Reaction score
3,153
CCM imara ni imani ya kiitikadi ndani ya mioyo ya Wananchi Watanzania,Awamu ya kwanza ya CCM iliyoongozwa na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ilikuwa ni ya kijamaa,kiongozi wa CCM akifanya ziara eneo fulani, basi Wananchi wanyonge walioonewa waliamini amekuja mkombozi wetu, na kwa hakika eneo hilo lilikombolewa,hii ilikuwa ni CCM Ujamaa iliyoasisiwa na Hayati Baba wa Taifa la Tanzania,Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na hiyo ndiyo imani ya Wananchi na amani ya taifa hili ilipo, wapo wanaotekeleza kwa vitendo imani ya CCM ya Ujamaa lakini wapo CCM Mabepari awa ni tofauti na CCM Ujamaa,CCM Mabepari hawako tayari kugawana mkate na mtu yeyote yule.

-Bila CCM imara Taifa litayumba.

CCM imara ni imani ya Ujamaa iliyo ndani ya Wananchi wa Tanzania,nimpongeze Katibu Mwenezi Taifa,Komredi Paul Makonda kwa kuturudisha kwenye misingi ya Ujamaa,alipofanya ziara kila eneo ilionekana Falsafa ya kijamaa na wokovu kwa wanyonge,tumsikilize kwa nukuu hii;-Katibu wa Itikadi na Uenezi,wa CCM Taifa,Ndugu Paul Makonda anamwagiza Waziri,akitumia mwavuli wa CCM na kuwa hayo anayomwagiza ni maelekezo ya chama,Katibu Mwenezi Paul Makonda anauliza: "Leo ni lini?" Umati unaitikia: "Jumamosiiii."
Waziri kwenye simu naye anajibu: "Jumamosi."Kisha,Katibu Mwenezi Makonda anampa amri Waziri: "Kesho naondoka Geita, tupishane na wewe ukiwa unaingia Geita."Ni amri ya Katibu Mwenezi Paul Makonda kwa Waziri, kwenda kushughulikia mgogoro wa ardhi katika vijiji nane mkoani humo,Hii ndio imani ya Wananchi kwa CCM kuona matatizo yao yanatatuliwa,kuna watu wanalaumu kwa nini Mwenezi Makonda anatoa amri!?,hii haikuwa mbaya kwa sababu Mwenezi alikuwa anatimiza matakwa ya Chama kuisimamia Serikali,mwenye Ilani ya Uchaguzi ni Chama Cha Mapinduzi,kwa nafasi yake kama Muenezi alikuwa sahihi kutoa maelekezo naaagizo kwa watendaji wa Serikali.

-Uteuzi wa Mwenezi Paul Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Kwa falsafa ya CCM Ujamaa nieleze mtazamo wangu kwa imani na Itikadi ya Ujamaa ulioasisiwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,Kwa mtazamo wangu Mh Rais ana watu makini wa kumsaidia na huenda hata hiki kilichofanyika ni kwa ajili ya maslahi mapana ya taifa,nirejee kukumbushana na wanaCCM wenzangu kuwa ndani ya Chama kuna CCM Mabepari na CCM Wajamaa sasa hii CCM Mabepari ni tofauti na CCM Ujamaa ambayo hiyo ndiyo iliyoasisiwa na waasisi wa taifa hili na hiyo ndiyo imani ya wananchi na amani ya taifa hili ilipo,kwa mtazamo wangu Mh Makonda alikuwa anatekeleza kwa vitendo imani ya CCM ya Ujamaa tatizo CCM Ubepari hawezi kukubali kugawana mkate na mtu mwingine yaani wao ni wabinafsi, ninaamini kuwa bila CCM imara taifa letu litayumba na CCM imara siyo majeshi tu bali imani ya kiitikadi ndani ya mioyo ya wananchi.

Kiongozi wa CCM akifika sehemu wananchi walioonewa waamini amekuja mkombozi wetu hilo tukilikosa tutalia,imefikia mahala wananchi wanaamini kuwa wapo viongozi ndani ya CCM wnatamani Chama kianguke kipandishwe Chama cha kibeberu na kibepari ili wao waingie madarakani na waongoze nchi yaani,sasa ikifika hapo tutaikumbuka CCM hii ambayo ilijenga hii nchi kwa jasho na damu. Mungu ibariki Tanzania na viongozi wake wote wenye mioyo na nia njema kwa taifa hili.

Nimalizie kwa kusema kwamba ni wakati wa chama chetu cha Mapinduzi CCM kuwa na politics counter interagency ya kutosha katika kulinda imani na itikadi ya chama chetu cha Mapinduzi CCM kwa watanzania tuliokula nao kiapo,siku CCM ikijisahau na kukiacha kiapo hiki kwa wananchi basi tuombe Mungu watanzania hawa wasije kutuhukumu maana tutakuja kulia na kusaga meno, ni vyema sasa vijana wazalendo wenye kukipigania chama kwa moyo na kauli thabiti wakapewa uangalizi mkubwa kwa uhai wa chama chetu cha mapinduzi CCM na Tanzania yetu,ni vyema pia siasa za visasi kwa baadhi ya wanasiasa nguli ambao wengine umri umekwenda na wengine vijana wakawa na mioyo ya mitume na manabii ya kusameheana na kujenga upendo kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo,kama taifa na chama chetu cha mapinduzi CCM kitajaribu kuyapa mgongo maswala ya chuki na visasi ndani ya chama chetu pendwa niwazi tutapanda mbegu itakayotuhukumu siku moja na kutusambaratisha kwani Mungu wa rehema atachoka kutuvumilia kwa ujinga na upuuzi wetu tulipkumbatia kwa roho na nafsi za kishetwani kwa manufaa ya watu wachache.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of business administration in International business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-
-Assessment on the Effects of Micro-financing on Poverty Reduction.
 
Hii picha ina trend sana. Uchumi wa Tanzania uko mikononi mwa watu wachache,wengi wanaishi maisha ya hali ya chini sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…