CCM ujana ni sifa ya ziada lakini CHADEMA ujana ni maisha yao. Sijajua UVCCM wanafeli wapi?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Ni kawaida sana kumuona diwani, mbunge au Waziri wa CCM akitamba kwamba sasa kazi itafanyika kwa sababu yeye ni kijana.
Na unaweza kukuta hata Kigwangalla au Shinza akijinasibu kwamba yeye ni kijana.

Lakini Chadema vijana hawanaga hizo swaga wao utawatambua kwa matendo yao tu kuwa ni vijana na wakati mwingine unaweza kujisahau ukamwita Sugu kijana kwa zile " pamba" anazopigilia.

Leo asubuhi nimemwona mbunge Nusrat aliyekuwa boss wa Bavicha nikamsahau kabisa nikadhani ni bi Fayza.

Kiukweli Freeman Mbowe ana uwezo mkubwa wa kuwekeza kwa vijana, kijana siyo hadi utuambie kuwa wewe ni kijana yatupasa sisi wenyewe kuliona hilo.

Mtu kama babu Tale anajiita mbunge kijana kuliko wote huku nyumbani ana watoto 7. Ingetosha tu aseme yeye ni mbunge mdogo kwa umri kuliko wote mbona tungemwelewa tu

Jafo naye waziri kijana.

Duh.....niishie hapo.

Kazi Iendelee!
 
Mwigulu Nchemba wa 1965 lakini bado anajiita kijana, sijui ukiwa kijina inatusaidia nini kama taifa kama siyo upumbavu, mwisho naona posho ya April bado haijazama mkuu maana bado upo normal kabisa
 
Hii inathibitisha kuwa dunia inaenda kasi Sana,kwa kukiri hilo.Chukua pepsi hapo kwa mangi bill yangu.
 
Bwasheee vp Palamagamba yupo au naye kawa kama Bashiru?
 
Mkuu ukiwa huko ubongo unapata mvi...mambo anayeaafiki aseme ndiyooo..huo ni uzezeta
 
Jamaa wewe na vistori vyako. Mpaka Lissu alipotamka yeye mwenyewe ana miaka 52 mimi kada mfuasi wake mwandamizi nilikuwa najua hafikishi hata miaka 45. Kutokana na swagga zake kila siku kuburuzana na polisi, kukatiza vichaka kukimbizana na wasiojulikana.
 
Aisee umefanya siku yangu kunoga sana!
 
Khahahhaaa mkuu ndio ukweli. Sisi vijana wa Mbowe hatuzeeni akili wala mwili. We are fit forever. Mwangalie Prof Baregu then ulinganishe na Steven Wasira[emoji28][emoji28]
Kwa kweli ni nyeusi na nyeupe
 
Una maana Jafo vipusa wanne?!😂😂! Baptist Wewe mbaya!
 
CCM wanapenda kujiita majina ambayo hayasadifu maisha yao. Hata mzee mgaya anajiita kijana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…