CCM: Utaratibu wa mtu mmoja cheo kimoja kufutwa

CCM: Utaratibu wa mtu mmoja cheo kimoja kufutwa

Mpinzire

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2013
Posts
7,503
Reaction score
13,463
CCM inaenda kubadikisha katiba yake! Kwa habari zilizopo CCM inaenda kuwarudisha makati tawala kuwa wajumbe wa NEC, Utaratibu wa Makatibu Tawala kuwa wajumbe wa NEC uliondolewa na Hayati Magufuli baada ya kubadilisha katiba na wajumbe wa NEC kupatikana kwa njia ya kuchaguliwa kikanda.

Sasa CCM imeamua kurudi kwemye utaratibu wake wa awali ambapo Makatibu Tawala ambao ni wateule wa Mh Rais watakuwa ni wajumbe waNEC moja kwa moja.

Pia CCM itabatilisha kifungu kilichoingizwa na Hayati Magufuli kuwa mtu anaweza kuwa na vyeo viwili tofauti bila shida, utaratibu huu pia ulifutwa kipindi cha Hayati Magufuli ambapo alitaka mtu mmoja cheo kimoja na ndipo kwenye uchaguzi mkuu 2020 wakuu wa mikoa walikuwa wanagombea walifutwa kazi.

Samia ataweza kurudisha Rasimu ya Warioba kwa utaratibu huu?

20220314_081339.jpg
 
"Kula kwa urefu wa kamba" hawa mbuzi kila siku naona wanahangaika kuongeza urefu wa kamba zao, ipo siku hizo kamba zitakatika mbuzi wataenda kula hadi kwenye meshamba ya wakuma, ndo utakua mwanzo wa mitafaruku na ukinzani kuanzia kwa mbuzi wenyewe hadi kwa mwenye mbizi.

Sijui kama ni meeleweka hapo, great thinkers
 
Hii serikali ni ya mawazo yakipigaji..yaani fursa zipo kidogo kwanini mrundikiane vyeo watu wachache??
 
"Kula kwa urefu wa kamba" hawa mbuzi kila siku naona wanahangaika kuongeza urefu wa kamba zao, ipo siku hizo kamba zitakatika mbuzi wataenda kula hadi kwenye meshamba ya wakuma, ndo utakua mwanzo wa mitafaruku na ukinzani kuanzia kwa mbuzi wenyewe hadi kwa mwenye mbizi.

Sijui kama ni meeleweka hapo, great thinkers
Shamba la bwana heri na mbuzi wa bwana heri !! Hapo hapatakuwa na shida mkuu !!
 
Hii ni fursa adhimu kwa Chadema kurudi kwenye ubora wao, maana kiongozi mwenye vyeo vingi lazima utendaji wake utakuwa mbovu sana.

Cdm haijawahi kushuka ubora, bali walihujumiwana mlevi wa madaraka.
 
Ni upumbavu wa hali ya juu kumuacha mwendawazimu mmoja anabadiri katiba na kanuni kwa utashi wake na bado walikuwa wanampigia makofi, pumbavu kabisa.

Bila Mungu kuingilia kati Magufuli alikuwa anaipeleka nchi kuzimu, ni bora amekwenda yeye kuzimu nchi imebaki.
 
"Kula kwa urefu wa kamba" hawa mbuzi kila siku naona wanahangaika kuongeza urefu wa kamba zao, ipo siku hizo kamba zitakatika mbuzi wataenda kula hadi kwenye meshamba ya wakuma, ndo utakua mwanzo wa mitafaruku na ukinzani kuanzia kwa mbuzi wenyewe hadi kwa mwenye mbizi.

Sijui kama ni meeleweka hapo, great thinkers
nimeelewa tu hapo kwenye "wakuma, meshamba na mbizi"
 
Matayarisho ya Uchaguzi ujao..., Alisema mama kwamba watu wapo kwenye matayarisho (alichosahau labda ni kusema) watu tupo kwenye matayarisho..., Kwahio huenda haikuwa fair kuwapiga nyundo hao wengine
 
Hii ni fursa adhimu kwa Chadema kurudi kwenye ubora wao, maana kiongozi mwenye vyeo vingi lazima utendaji wake utakuwa mbovu sana.
Na wewe katibu Tawala unaenda kula mashavu mawili. Wale chawa wengine waendelee kusugua benchi tu.
 
Back
Top Bottom