G Jonathan Kamenge
Member
- Apr 8, 2023
- 30
- 23
Katika wimbo wake mpya, Mwanamuziki Roma Mkatoliki amekilinganisha Chama Cha Mapinduzi na Maandazi na kudai ikiwa atatakiwa kuchagua, atachagua Maandazi badala ya CCM. Siyo lengo kumjadili Roma kwa vile simfahamu binafsi, bali kujibu hoja ikiwa "Kupitia Dola, Serikali imeua hari ya vijana kutaka kushiriki Siasa za taifa lao!!?". Nilisema katika Makala iliyopita kwamba wengi wa washajihishaji wa hoja hii, wanadai "kutekwa" kwa Roma Mkatoliki ni moja ya vitu vimewatisha vijana.
Ebu tujaribu kufikiri. Kwanza ni juu ya ukweli kwamba hakujawahi walau kwa miaka ishirini iliyopita, kuwako na ukandamizaji wa Demokrasia nchini, hii ni kama tutaamua kuwa wakweli kwa nafsi zetu badala ya kuhemkwa na propaganda za makundi maslahi ya kisiasa na uingiliaji wa mashirika "ya Kimataifa" katika Siasa za Afrika.
Ngoja niweke ushahidi kidogo hapa. Wakati Hayati Benjamin William Mkapa akituhumiwa "kukandamiza" Uhuru wa vyombo vya habari, tunasahau ni wakati wa Utawala wake na kwa yeye mwenyewe kuwashawishi Agakhan kufungua Magazeti ya Mwananchi hapa nchini. Huenda hatukujua au tumesahau.
Mh. Jakaya Mrisho Kikwete alilalamikiwa "kukandamiza Demokrasia" lakini ndiye Rais aliyekutana na mashambulizi makali ya "uhuru wa maoni na habari nchini" kiasi wakati Wanasiasa wakimwita "Dhaifu", wanahabari wa vyombo vikubwa na sisi wengine waandishi wa Makala mitandaoni tuliandika na kutengeneza kila aina ya conspiracy theories wakati wa Utawala wake. Tulisema waziwazi na bila haya kwamba "tunahitaji Rais Dikteta na asiyechekacheka hovyo" wengine wakienda mbali zaidi na kusema "asiyechekacheka kama shoga" na "Mzee wa Msoga" kama kawaida yake akacheka na kutuacha tuseme. Alikuwa na kazi moja tu, kuwa Rais na siyo kusutana na wakosoaji wake, na hilo alilifanya vyema.
Kisha CCM kama kawaida yake ikasikia "kilio" cha wananchi kutaka "Rais Mkali, Dikteta, atakayetupeleka mputamputa" na Kikwete hakuwa Nabii alipotwambia "wameleta chuma kinachotema chche".
John Pombe Magufuli yeye akajionyesha kuwa "the No nonsense President" karibu kwenye kila eneo la Utawala wake, lakini wakosoaji hatukuacha kumkosoa, hatukuacha kuandika na kumchora, ni Upumbavu mkubwa kudai kuna mtu alitekwa kwa sababu alikuwa anakosoa Serikali, siyo Tanzania. Nasema hivi kwa ujasiri kwa sababu kwa zaidi ya miaka kumi na tano nimeandika na kukosoa kwenye maeneo mengi Serikali ya Tanzania katika awamu zote, na sikuwahi kutekwa ama kutendewa vibaya. Ushahidi uko, Makala zangu ziko Facebook na kwenye blogs kwa miaka mingi na sikuwahi hata kuhisi kwamba pale nilipokinzana na vyombo vya Dola (and trust me I have had my share), ilikuwa ni kwa sababu nakosoa Serikali, ilikuwa mara zote ni kwa sababu baadhi ya watendaji walitaka ama kuvunja haki zangu ama za wengine kwa maslahi yao binafsi, na mimi sikuumbwa na uvumilivu wa uonevu. Naamini kwenye ama kuuondoa Uovu kwa mkono wangu, kuukemea kwa kinywa changu ama kuuchukia moyoni mwangu.
Sasa tuwe wakweli, Uhalifu wa watu kuuana, kutekena, kushambuliana, na hata kujiteka na kutafuta "kiki" kupitia matukio ya kawaida kabisa ni moja ya mambo yameshuhudiwa sana hasa wakati wa awamu ya Tano ya Serikali. Wakati wengi tunakumbuka "kutekwa" Roma Mkatoliki, na kushambuliwa Tundu Lisu, tunakumbuka pia kuumia Mwenyekiti wa chama kimoja hivi na kudai kashambuliwa na hatimaye kugundulika kwamba "alishambuliwa" na mizinga kadhaa ya Konyagi kama siyo K-Vant alizozifakamia akisahau yeye ni public figure.
Vyovyote iwavyo, nadhani ambacho kiliminywa hapa katikakati siyo "uhuru wa kukosoa serikali", bali uhuru wa "kumwaga mitusi" na kukosa staha katika ukosoaji wetu. "Mwanaharakati Huru" anayekaribia kufirisiwa baada ya kushindwa kesi mahakamani kwa sababu ya "kufanya harakati bila staha Wala busara" ni mfano mzuri. Huwezi kutumia "Uhuru" wako kuwatusi, kuwadhalilisha na kuwakosea adabu viongozi wa Serikali na jamii halafu ukataka Serikali na mahakama visikuwajibishe kwa sababu "una uhuru wa maoni". Nadhani Iko tofauti ya kuwa na maoni na kuwa na ama mihemko inayokufanya kumwaga mitusi, ama kuwa na Hila za kutengeneza matukio halafu utafute "umaarufu wa harufu" kwa mgongo wa "naonewa kwa kukosoa".
Rais wa sasa, Mheshimiwa Samiah Suluhu ametutaka sote "kumkosoa" na kusisitiza kwamba tunapomkosoa tunamsaidia kuona mahala penye mapungufu na kuyafanyia kazi, mbaya ni hatuna wakosoaji tena, na wamwaga mitusi wanaogopa kumwaga mitusi kwa vile wanajua "msumeno" ukatao kuwili umenolewa, tayari kukata pande zote.
Ha ha ha ha!! Hii gemu haitaki hasira.