nyamadoke75
Member
- Apr 1, 2020
- 93
- 288
Wakati Joto la Uchaguzi likizidi kushika kasi hapa nchini, Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Arusha tayari kinadaiwa kupanga safu ya siri ya wagombea udiwani katika kata sita huku Mrisho Gambo akizidi kucheza rafu kuhakikisha nafasi ya Ubunge anashinda mapema asubuhi.
Licha ya kutoanza kinyang'anyiro cha kura za maoni baadhi ya makada wa CCM wanaowania kata hizo wameibua taharuki wakibainisha kwamba iwapo mpango huo utafanikiwa chama hicho kipo katika hatari ya kupoteza kata hizo.
Habari za kuaminika zimedai kwamba mpango huo unaratibiwa na mtaalamu wa fitina, Mrisho Gambo kwa kushirikiana na Mwenyekiti Wa CCM Wilaya, Joseph Massawe, lengo ni kuhakikisha wale wanaowahitaji wanapita ili kumsaidia Gambo katika kinyang'anyiro cha Ubunge baada ya kuahidiwa nafasi ya Uwaziri.
Makada wanaodaiwa kugawiwa kata hizo ni pamoja na Ally Meku (kata ya Kati) Sakina Mpufu(Olorien) Issa (Ungalimited) Abraham Mollel (Kimandolu)pamoja na Mary kisaka ambaye amepewa nafasi ya ubunge wa viti Maalumu.
Hata hivyo Gambo amewaahidi kuwapatia Pikipiki Makatibu wote wa kata na Wenezi wa CCM katika kata zote jijini Arusha iwapo watampa ushirikiano katika nafasi ya Ubunge na tiyari pikipiki hizo zimeshaingia zikisubiri mpango ukamilike waweze kugawiwa.
Gambo mpaka sasa amefanikiwa kwa kiwango kikubwa kumweka mfukoni mwenyeviti wa ccm wilaya ,Joseph Masawe na Mwenyekiti Wa Ccm Mkoa Wa Arusha ,Zelothe Steven ambaye ushindi wake wa nafasi hiyo ulifanikishwa na Gambo pamoja na Catherine Magige kwa lengo la kuwasaidia katika mambo yao ya Ubunge.