VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Kwa takribani siku sita,kulikuwa na mjadala juu ya Vifungu vya 37 na 38 vya Kanuni za Kudumu za Bunge la Katiba.Vifungu husika vinahusu namna ya kufikia uamuzi Bungeni kwa njia ya kupiga kura pale ambapo kutakuwa na haja ya kufanya hivyo. Kura zitapigwa hata wakati wa kupitishwa kwa kifungu kwa kifungu cha Rasimu ya Pili ya Katiba itakayojadiliwa na kupitishwa na Bunge.
Mvutano wa wazi na mkali ulikuwa juu ya Kura ya Wazi au Kura ya Siri. CCM katika mjadala mzima ilishindwa kuwashawishi Wajumbe waiunge mkono katika kuipigia upatu kura ya wazi. Mjadala ukawa mgumu na kuahirisha Bunge mara kwa mara. Ndipo ilipoundwa Kamati ya Maridhiano kushughulikia suala hilo.Hata Kamati nayo ikagonga mwamba katika kuamua.
Leo asubuhi,Bunge la Katiba limepitisha Kanuni husika likiviacha vifungu vya 37 na 38 kama vilivyo.Ikatolewa taarifa kuwa Kamati ya Maridhiano itashughulikia suala hilo. Hapo ndipo CCM iliponyakua ushindi. Baada ya kesho kuchaguliwa kwa Mwenyekiti wa kudumu wa Bunge la Katiba na Bunge kuanza kazi yake ipasavyo,maamuzi mengi na mamlaka yatakuwa katika kiti cha Mwenyekiti.
Kamati ya Maridhiano italazimika kumwachia Mwenyekiti aamue kuhusu suala hilo kwa kutumia busara zake. Iko wazi kuwa Mwenyekiti wa Kudumu atatokea CCM.Hii ni kwa kuangalia idadi wa Wajumbe wenye mafungamano na CCM. Hivyobasi,kuna uwezekano mkubwa Mwenyekiti huyo kutoka CCM akasimamia msimamo wa chama chetu wa kura ya wazi wakati wa kupitisha Rasimu ya Katiba. Na hapo ndipo mchezo utakapoishia.....
Mzee Tupatupa wa Lumumba (sasa Dodoma)