Black Jesus
JF-Expert Member
- Mar 7, 2008
- 256
- 10
CCM wajiandaa kujibu kauli ya Anne Kilango kuhusu kuogopa mafisadi
Na Kizitto Noya
KAULI ya Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango kuwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanaogopa kupambana na ufisadi kwa kuwa mafisadi ni viongozi wenzao, inaonekana kukikera chama hicho na sasa kinaandaa taarifa maalum kujibu mapigo.
Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana, Katibnu Mkuu wa chama hicho, Yusuf Makamba alisema ingawa suala la ufisadi limejadiliwa vya kutosha katika jamii, atalazimika kuandaa taarifa kujibu kauli ya Kilango na kuikabidhi kwa katibu mwenezi wa CCM ili aitoe kwa vyombo vya habari.
"Haya mambo yanaandaliwa, hatukurupuki tu na kujibizana magazetini. Ninaandaa taarifa na baada ya Sikukuu ya Pasaka mtafute katibu mwenezi akupe ufafanuzi wangu," alisema Makamba.
Makamba alitoa kauli hiyo baada ya kusita kwa muda kuzungumzia suala hilo akidai kuwa yaliyosemwa kuhusu ufisadi, yametosha na jamii sasa inapaswa kujadili mambo mengine ya maendeleo.
"Niache, mimi niko likizo ya sikukuu na najiandaa kwa uchaguzi wa jimbo la Busanda. Ukitaka tuzungumzie uchaguzi huo kwa kuwa ndiyo suala jipya," alisema Makamba na kuongeza:
"Suala la ufisadi limepitwa na wakati, kwani limejadiliwa sana na mengi yamezungumzwa, na hata CCM imejitahidi kueleza," alisema.
Makamba alieleza hayo alipotakiwa kueleza msimamo wake akiwa Katibu Mkuu wa CCM kuhusu kauli ya Kilango kwamba viongozi wa CCM wanashindwa kuwafichua mafisadi, kwa kuwa miongoni mwa wanaotuhumiwa wamo wabunge, viongozi na wanachama wenzao.
Kilango alitoa kauli hiyo juzi alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Tuongee Asubuhi, kinachorushwa hewani na kituo cha Televisheni cha Star na kueleza kuwa ugumu wa viongozi wa CCM kupambana na mafisadi, upo katika ukweli kwamba, wanaopambana nao ni viongozi wenzao.
Bila ya kutoa mifano bayana, Kilango alisema ni wabunge wachache wanaoweza kusimama kidete kutetea sura ya nane ya Ilani ya Uchaguzi wa CCM inayozungumzia vita dhidi ya ufisadi na hii inatokana na mahusiano yaliyopo kati ya watuhumiwa na viongozi hao.
"Ugumu wa sura ya nane ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ni kwamba, unapambana na mwanachama mwenzako, mbunge na hata kiongozi. Na hii ndio inawafanya watu wengi kushindwa isipokuwa wachache kama mimi," alisema Kilango na kuongeza.
"Unaposimama imara kutaka kufanya mabadiliko kutetea haki na kupinga ubatili, unapaswa kutegemea mengi na mimi niliyategemea na ndio maana sipati tabu katika vita dhidi ya rushwa na ufisadi".
Alisema viongozi wa wananchi wa Tanzania wanapaswa kuwa wakweli na wawazi katika kupinga rushwa kama wanavyofanya watu wa Marekani.
"Nchini Marekani mtu aliyetaka kurithi nafasi ya useneta wa Obama alitanguliza rushwa ili kuwashawishi wajumbe, jambo ambalo liliwafanya Wamarekani kusimama imara na kuzungumza ukweli kuhusu kashfa hiyo," alisema Kilango ambaye alipata tuzo ya Mwanamke Jasiri aliyopewa na Serikali ya Marekani hivi karibuni.
Alisema jamii inapaswa kuwaunga mkono kwa nguvu zote wachache waliothubutu kuikemea rushwa nchini.
Katika kashfa nyingi za ufisadi, viongozi na wabunge wa CCM ndio wamekuwa wakituhumiwa kuhusika na miongoni mwa waliofikishwa mahakamani ni viongozi wa zamani katika serikali ya CCM, huku moto dhidi ya wabunge wa sasa ukizidi kuwaka katika kashfa za miradi mikubwa.
Miongoni mwa miradi hiyo ni ununuzi wa rada, ambao umeelezwa kuwa ulifanywa kwa kuongeza bei ili iwe juu kwa lengo la kujipatia kamisheni nzuri. Miradi mingine ni wa uzalishaji umeme wa dharura wa Richmond uliosababisha mawaziri kujiuzulu baada ya kutajwa kwenye ripoti ya kamati teule ya bunge na wa uzalishaji umeme kwa kutumia makaa ya mawe wa Kiwira.
Kashfa nyingine iliyohusisha wanachama na viongozi wa CCM ni wizi wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), katika benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambayo inahusisha majina ya vigogo wanaohusishwa na kampuni zilizochota fedha nyingine, lakini imekuwa ni vigumu kuwataja.
Hata hivyo Kilango hakutaja majina ya watu wanaojaribu kuwazuia au kuwamaliza, bali aliapa kuendelea na vita hiyo kwa kuwa hayo ni maumbile na hulka yake.
"Mimi ndivyo nilivyozaliwa na ni maumbile yangu kuzungumza ukweli. Rangi nyekundu nitasema kuwa ni nyekundu na bluu pia, wala hakuna mtu atakayeweza kuninyamazisha ili niseme kuwa ni nyeupe, kibaiolojia siku zote naweza," alisema na kuongeza:
"Wapo wapole, waoga ambao hata chumbani kulala peke yao wanaogopa, lakini pia wako majasiri wanaothubutu".
Alisema Watanzania walishachoshwa na rushwa na kufikia hatua ya kujenga imani kuwa wabunge wa CCM wapo kwa ajili ya kuilinda serikali yao na wanaoweza kuikosoa ni wabunge wa upinzani tu.
"Sasa wananchi wa Tanzania wanapaswa kuondoa imani hiyo na sisi tupo kwa ajili ya wananchi na msimamo wangu, chama hakiwezi kupendwa kama hakikosolewi. Tukikosoa ndio tunakipa afya na si kukidhoofisha kama wanavyodhani baadhi ya watu," ailsema.
Alifafanua kuwa vita dhidi ya rushwa ni kama mashindano ya riadha kwani kuna wanaoanza wanaoshindwa katikati, wanaomaliza na pia kuna wasiothubutu kuanza.

Last edited: