Mpka sasa hivi CCM wakitaka wabaki madarakani wazingatie yafuatayo.
1. Waufute mfumo wa kutumia CHAWA kwasababu wamekinaiwa na wananchi na hawapendwi tena kwahiyo hawana ushawishi no more.
2. Katika kura za maoni wawapitishe wagombea ambao ni wapya madarakani wasiwe wale ambao wameshahudumu kwa muda mrefu kwasabab wananchi hawana tena imani nao.
3. Wagombea watakaopitishwa kwenye kura za maoni wawe wasomi, wenye ushawishi na uwezo halisi wa kuongoza wasiwe wanapayuka na kutoa sera za ki CHAWA wakiwa majukwaani. Wateme sera za kisomi na ambazo zina reflect matamanio ya WATANZANIA.
4. Watekeleze miradi kikamilifu ndani ya hii miezi michache ilobaki mpka kufikia uchaguzi, ikibidi kamati za kisiasa katika maeneo husika zivunjwe wawekwe watu wasio na tamaa na wajanja wajanja, watu hawa wapewe majukumu ya kusimamia miradi ikamilike kabla ya October.
5. Wapunguze kutumia nguvu na kuvunjwa katiba, kwasabab hivi vitendo vinazidisha sumu kwa WATANZANIA na wakisha amka na kuthubutu kufanya yao basi CCM ndo itakuwa mwisho wao.
6. Kwanzia ngazi ya Taifa mpka vitongoji Kwa zaidi ya asilimia 85 ya viongozi kutokew CCM hawana uwezo halisi wa kiuongozi kwanzia kichwani mpka ki muonekano na kimatamshi ndiyo maana huishia kuwa CHAWA na kulopoka hovyo. Kifupi wasiofaa wapo madarakani na wanaofaa wapo kwenye mbao ndefu.
Conclusively, CCM ibadilike, ndani ya chama kuna watu smart sana na wanauwezo mzuri ila hawapati nafasi kwasabab ya mfumo mbovu katika kura za maoni. Yani kifupi ni anayechaguliwa kigezo ni awe CHAWA mzuri asiye na aibu, awe na uwezo wa kujichetua akili, awe mzuri kushawishi watu kupitia njia zisizofaa, n.k
Mfano.
Arachuga yule bwana akili hana
Ofis ya prezoo wizara ile yule mtu uwezo ni mdogo
Dar yule mtu akili kichwani ni ya kawaida sana IQ ni ndogo
Mwenezi naye ni walewale IQ yake ni hakuna kitu
Wabungwee ndo usiseme sasa....ni aibu
Mimi nimesoma na mjukuu wa aliyekuwa mbunge wa jimbo flani kanda ya magharibi, yule kijana alikuwa mchoyo sana yani nikisema mchoyo nieleweni ni exceptional siyo uchoyo wa kawaida ni uchoyo wenye ushetani ndani yake.
Lakini saivi namuona anasimama majukwaani anatafuta fursa za kiuongozi kifupi ni kwamba yule dogo akipata cheo kuhudumia wananchi basi taifa litakuwa limeongeza idadi ya mafisadi. Namuomba mungu yule dogo asije kushinda post atakayogombea🤲🤲🤲