JK sijui kama anapata usingizi..maana Dr.Slaa ni chuma haswa sijui atamkabili vipi.mi natamani waweke mdahalo nione JK anavyoweweseka na kuwekwa kati
== Kabla ya kuamua kuitupilia mbali hoja ya mgombea binafsi wa urais?
... waliogopa kuwepo watu waliomashuhuri na kuaminika kuweza kumpiku urais Mh. Kikwete?
... waliogopa kura kutawanyika sana na mmoja wa wapinzani angeliweza kushinda uchaguzi?
== Kabla ya Chadema kumteua Mh. Slaa kuwawakilisha kwenye kiti cha urais?
... walijua ni Ndg. Mbowe ndiye atakaye wawakilisha Chadema?
... walidhani Mh. Slaa hatokubali kupoteza kiti chake cha ubunge kwa kimbilio la urais?
Naomba mnisaidie kuyajibu haya, ahsanteni.
Steve Dii
Hakika mpaka sasa mauzo ya handkerchief na tissue yatakuwa yameshamiri vibaya sana kwa joto aliloleta Dr. Slaa na kuendelea kulikoleza dhidi ya himaya ya CCM!!
Hivi waliliona hili, strategists wao lazima walikuwa wamelala kutoruhusu hukumu ya mgombea binafsi ishinde. Itakula kwao na kuzidi kumega zaidi...
== Kabla ya kuamua kuitupilia mbali hoja ya mgombea binafsi wa urais?
... waliogopa kuwepo watu waliomashuhuri na kuaminika kuweza kumpiku urais Mh. Kikwete?
... waliogopa kura kutawanyika sana na mmoja wa wapinzani angeliweza kushinda uchaguzi?
Naomba mnisaidie kuyajibu haya, ahsanteni.
Steve Dii
sidhani kama ccm ilikuwa ina wasi wasi sana hivyo kwenye upande wa rais (at least before Slaa kutangaza nia).Wasi wasi wazo zaidi ni nafasi za ubunge na nafasi nyengine za serikali za mitaa.
Wanajua kuwa kutoa nafasi ya wagombea binafsi, wangeibuka watu wanaokubalika ndani ya jamii ambao hawataki kujiunga na siasa za kichama na hivyo kupunguza idadi ya viti vya ccm bungeni.
Wanajua kuwa chama chao kina majungu na makundi, na ingekuwa njia nyepesi sana kwa waliochoshwa kujiengua na kujichotea kura ambazo ingepigiwa ccm