CCM wamejipanga vipi kukabiliana na timu tano?

CCM wamejipanga vipi kukabiliana na timu tano?

Tuko

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2010
Posts
11,180
Reaction score
7,346
Msimamo wa CCM wa kutaka srikali mbili unatarajiwa kuibua mtifuano mkali sana siku chache zijazo.

Msimamo wa CCM unatariajia kupata upinzani mkubwa sana ndani na nje ya bunge kutoka katika timu zifuatazo

1. Wazanzibari - Wanataka serikali tatu na wana 'nguvu' kubwa kama mshirika mwenza kwenye muungano

2. Wapinzani - Wanataka serikali tatu na wana nguvu kubwa sana kwa kuwa wanaungwa mkono na majority of middle class people ambao wanasauti kubwa kupitia vyombo vya habari

3. Wazee wa chama - Ingawa Mukama na Nape waliua nguvu yao kwenye chama, lakini tumeona ushawishi mkubwa sana kwa wazee hawa ambao wengi wapo kimya (isipokuwa Kingunge) lakini ni wazi kuwa watamuunga mkono mzee mwenzao Warioba

4. Wananchi - Wamenena kupitia maoni yao kwenye rasimu kuwa wanataka serikali 3. Watakuwa na influence kubwa sana nje ya bunge

5. Tume ya marekebisho ya katiba - Wanatetea rasimu yao. Watasaidiwa sana na ushawishi wa watu kama Palamagamba na Butiku.

Tusisahau kuwa kamisaa wa mchezo (JK) nae anataka katiba mpya ipatikane na katika hilo anajua kuwa wakipeleka rasimu inayosema serikali mbili, itakuwa rahisi kwa ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko rasimu hiyo kukubaliwa kwenye kura ya maoni...
 
Asante kwa uchambuzi mfupi, lakini unaoakisi hali halisi iliyopo. Ukweli ni kwamba muungano wa serikali 2 umeshapitwa na wakati. Wanaoulazimisha ni sawa na kutaka kuurudisha umri wa mtu nyuma.Kama una miaka 50 huwezi kwa vyovyote vile ukarudisha miaka yako iwe 40. Wakati ukuta, ukijaribu kupigana nao utaumia mwenyewe.
 
Back
Top Bottom