UTAKUJA UJE
Member
- Aug 4, 2020
- 34
- 78
Kila nikimsikiliza Tundu Lissu, nashindwa kuamini kama kweli anayosema ni uwezo wake mwenyewe au kuna nguvu gani nyuma yake. Ukiachilia mbali uwezo na ukuu wa Mungu aliyemponya kifo,ukaachilia mbali ujasiri wake,jambo kubwa linalomfanya Lissu akubalike na azidi kupaa kisiasa ni serikali ya CCM chini ya utawala kandamizi wa John Magufuli,ntafafanua.
Magufuli na Serikali yake wamekuwa wakijipambanua kuwa Serikali ya wanyonge na mtetezi wao mkuu. Unajiitaje serikali ya wanyonge ilihali Rais pekee anatembea na maburungutu ya pesa kwenye gari na kuwagawia wananchi kila pahala apitapo kwa kisingizio cha kutatua kero.Pesa hizo ni mshahara wa Rais! Ni pesa iloyoidhinishwa na wabunge!Inakaguliwa na nani?Majibu yake hayajulikani-lissu anapeta
Serikali ya CCM chini ya Magufuli iliwatimua wanafunzi pale UDOM ambao wengi wao ni watoto wa maskini.Mbaya zaidi ni kauli chafu toka kinywani mwa magufuli,kwamba wale ni vilaza.Unajiitaje mtetezi wa wanyonge ilihali unafukuza watoto wa wanyonge na kuharibu kabisa ndoto zao-tundu lissu pasua anga
Magufuli na CCM yake wamedhulumu haki za wafanyakazi. Huongezi mishahara ya wafanyakazi miaka mitano,hupandishi madaraja,wewe ni mnyonga wanyonge-lissu tusua,fisiem wamefeli
Mtetezi wa wanyonge anatumia mabilioni ya pesa kujenga uwanja wa ndege chato na miundombinu mingine mingi bora.Huku ni kuwafanya wananchi mazezeta.Makao makuu ya mkoa wa geita ni geita mjini,ulishindwa nn kujenga uwanja huo geita hadi uupeleke kijijini kwako?Pesa zote hizo ziliidhinishwa na bunge lipi?-Lissu hapa hapa piga goli la kisigino.
Mtetezi wa wanyonge anayezuia soko huru kwa wakuli,ni mnyonga wanyonge. Wakulima wengi wa mazao ya biashara kama vile pamba,korosho,kahawa nk,hawana uhuru wa kuuza mazao yao.Wanapangiwa bei na serikali na bado wanakopwa.Mh lissu komboa nchi kwa kuwapa haki wakulima
Kitokacho kinywani mwa Magufuli sicho atendacho. Magufuli amekuwa mwingi wa kujinasibu kwamba maendeleo hayana chama.Huyu huyu amekuwa wa kwanza kuwatisha wapiga kura kwamba wasipochagua wabunge wa fisiem kamwe hawezi kuwapelekea miradi ya maendeleo kama maji,barabara,umeme nk,pesa zinazotekeleza miradi hii ni kodi za wananchi si za magufuli wala babake!-lissu mtimulie vumbi utinge ikulu
Serikali na Rais waliofanya mazuri,ya nini kuminya uhuru wa habari?Tv zote,kipindi hiki zinamnadi magufuli tu,demokrasia iko wapi?Sera za wagombea wengine tutazipataje?Bunge live wakafungia,wanaogopa nn?-lissu kamatilia baba,ikulu ni yako
Magufuli na CCM yake wanajimaliza wenyewe,wananchi siyo wajinga,hamchaguliki tena,na kama siyo ubabe mnaopewa jeuri na polisi,hamkustahili kupata hata jimbo moja!Imetosha!Mkapumzike-mitano kwanza,tunasafiri na Tundu Antipas Lissu-Rais atakayerejesha uhuru wetu kupitia katiba mpya