Mkimbizi
JF-Expert Member
- Aug 23, 2008
- 222
- 35
Jana nilikuwa napata kilaji mahala fulani, akapita omba omba fulani. Alivyokuja kwangu nikamwambia mimi hela hata nikikupa haitasaidia, cha maana October 31 usiipigie kura CCM. Nikamwambia akiipigia CCM ataomba omba maisha yake yote na vizazi vyake kwa maana gap kati ya mwenye nacho na asiyenacho ni kubwa na hakuna anayewajali. Akaondoka. Baada ya muda akapita dada anauza soksi etc, akaja kwangu, nikamwambia soksi zako kwa mazingira haya siwezi kununua. Yote hii ni sababu kuna mfumo duni na usiofaa kwa wachuuzi wadogo wadogo matokeo yake hamfanikiwi. Nikamuuliza umejiandikisha kupiga kura? akajibu hapana. Nikamwambia basi waambie rafiki zako na ndugu zako wasiipigie kura CCM maana utaishia kuuza soksi maisha yako yote wakati watu wanaishi maisha ya peponi.
Kumbe pembeni kulikuwa na kada wa CCM, akaanza kuongea kwa jazba(baada ya kuona reaction ya yule omba omba na dada muuza soksi)". ''wewe unaongea nini, sio kila mahala mtu anafurahia unachosema!!!''. Nikamuuliza kwani shida iko wapi mbona jazba..? Wewe hunijui mimi, mimi nakujua sana wewe unakuja sana hapa... Nikamwambia kwahiyo?? Nikaongelee ******? Yani upuzi wote miaka 49 toka tupate uhuru nikae kimya?? Mbona unatumia nguvu nyingi kuongea?? Mapovu, unatetemeka vipi bwana nchi huru hii kusema.. Au mmezoea kuendeshwa tu kama mapunda?? Jamaa akaondoka akabamiza meza na kunitisha..!
Sasa najiuliza, jazba jazba jazba.. Yule mwingine alitishia kumshtak mtu kwenye mdahalo TBC. Sasa tunajua na dawa yenu ni october 31 tu!!!