CCM wanafanya wanavyotaka. Tusipeane moyo wala maini

CCM wanafanya wanavyotaka. Tusipeane moyo wala maini

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
1,958
Reaction score
3,890
Huo ndio ukweli. CCM wanafanya wanavyotaka inavyoonekana kwa sasa wapinzani wamekaa kimya wakiangalia ni kwa jinsi gani CCM wanavyopapatuana, na yote haya ni kutaka kuudanganya umma kuwa sasa CCM na serikali yao wanafanya kweli katika kulijenga Taifa mwisho wa siku wanarudi palepale bora Magufuli tunaendeleza sera za CCM na tunasimimamia aliyoaanzisha Marahemu Magufuli.

Ukweli haujulikani wanafanya kitu gani.

Kama ni timu kwa jinsi ya pangua pangua aliyoingia nayo Mheshimiwa Rais Samia ni dhahiri CCM nchi imewaelemea vibaya sana, watake wasitake ubabaishaji umekuwa mkubwa huke siku zinayoyoma kuukaribia uchaguzi.

Kesho keshokutwa anaondolewa spika apishe uchunguzi kwa kuvunja katiba, yaani Serikali au tuseme CCM inahamisha fikra kila siku,inawahamisha wananchi kutoka kushoto kwenda kulia ni kuwachezesha kwata.

Na wananchi wamekuwa kama mazezeta.
 
CCM haitoki leo wala kesho madarakani. Chukua mfano, tangu Mama aingie madarakani, yeye pamoja na chama chake na serikali yake wamepata uungwaji mkono mkubwa hasa humu JF. Wale waliokuwa mstari wa mbele kupinga leo ndio wanahakikisha wanamsema vizuri Mwenyekiti wa CCM na Serikali yake kuliko wana CCM yenyewe. Tundu Lissu sio habari kwao tena. Chadema si kitu tena. Kwa hali hiyo, CCM itatawala DAIMA!
 
Milele na ndio maana WaZanzibari hawawaamini WaTanganyika katika kuing'oa CCM, tuseme ukweli wabara mnahadaika na hela kirahisi sana.
 
CCM haitoki leo wala kesho madarakani. Chukua mfano, tangu Mama aingie madarakani, yeye pamoja na chama chake na serikali yake wamepata uungwaji mkono mkubwa hasa humu JF. Wale waliokuwa mstari wa mbele kupinga leo ndio wanahakikisha wanamsema vizuri Mwenyekiti wa CCM na Serikali yake kuliko wana CCM yenyewe. Tundu Lissu sio habari kwao tena. Chadema si kitu tena. Kwa hali hiyo, CCM itatawala DAIMA!
Ukweli mtupu!
.
Haya majamaa yalishaelekea kibra tena yalijipeleka yenyewe, mama yeye ni kuvuta na kugonga tu.

Ccm daima
 
Ukweli mtupu!
.
Haya majamaa yalishaelekea kibra tena yalijipeleka yenyewe, mama yeye ni kuvuta na kugonga tu.

Ccm daima
sasa hivi ni CHADEMA daima maana wanalosema Chadema, mwenyekiti wetu mbio.
 
Shida ya mwendazake inaezakuwa moja tu, alikuwa hapendi kubandika mawe na kuwaambia watoto wachochee bila kufunua ndani,hapendi uongo, aliwazimia jiko kabisaa, rip ila bimkubwa anaweza[emoji23][emoji23],tena kuwakoleza kawatandikia na mkeka,yamejisahau yanashangiria.
 
Hili li chama ni balaa na laana kubwa sana kwenye hii nchi , yaani tuombe tu Mungu akichukue hiki chama kikawe cha malaika mbinguni ndio hii nchi itapona vinginevyo haya majitu ya kijani kibichi ni yaleyale akili zilezile.
 
Mabadiliko yataletwa na wewe mwenyewe

Back
Top Bottom