Ccm wanaiba rasilimali za nchi isiyo na serikali!

Anko Sam

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2010
Posts
3,254
Reaction score
903
Mimi sishangai viongozi CCM wanapo ng'ang'ania muundo wa serikali mbili, kwanza una manufaa makubwa kwao kwani wanaiba na kufanya ufisadi kama tunavyoshuhudia. Tangu serikali ya Tanganyika ilivyo disolve na kukabidhi kila kitu chake kwa serikali ya Jamhuri, kukawa hakuna ulinzi wa mali na rasilimali za Tanganyika. Kukawa hakuna wa kuisemea tena bali ilitegemea utashi wa Rais Jamhuri kuilinda ama kuivuna!

Rais Nyerere hakuwa na tamaa za kifisadi na alishawahi kusema "Katiba ya Jamhuri inamruhusu kuwa dikteta...", yaani anaweza kufanya chochote kwa nchi ya Tanganyika kwa sababu haina wa kuisemea! CCM ya sasa na viongozi wake wameamua kutumia mwanya huo kuifilisi Tanganyika kwa sababu haina wa kuisemea wala kuilinda! Hili Zanzibar walisha ligundua kitambo, waliona utawala unavyokwenda wakaona mafisadi wanaweza kuanza kuiuza nchi yao, ndiyo maana wao waka-amua kujizatiti kuilinda nchi yao na rasilimali zake mafisadi wasije tia mikono yao kule! Wakatunga katiba yao mpya, wimbo wa Taifa nk. Hivyo Mafisadi hawawezi kuuza hata kipande cha mti Zanzibar.

Kwa Tanganyika, mafisadi wanavuna na kuuza nchi wapendavyo maana ni nchi isiyo na serikali yake, hakuna wa kuilinda! Hawaionei uchungu wowote zaidi ya kujinufaisha wao na mabwana zao. Wanatwambia sera ya ubinafsishaji ina manufaa, wakati tunashuhudia viwanda vinakufa, ardhi na mbuga zinauzwa, wanaingia mikataba ya kinyonyaji wao wanapewa share na sisi wananchi wa kawaida hali inazidi kuwa mbaya!

Kama CCM inataka serikali mbili, basi tubadilishane, Tanganyika iwe na serikali yake na Zanzibar idisolve nchi yake na iongoze Serikali ya Jamhuri kwa miaka 50 ijayo! CCM AU ZANZIBAR WAKIKATAA SHARTI BASI LIWALO NA LIWE!

Kwa kifupi Watanganyika tunasema: CCM INAFISADI NCHI KWA SABABU TANGANYIKA HAKUNA SERIKALI YA KULINDA RASILIMALI ZA TAIFA! Serikali ya JMT kazi yake ni yale mambo saba yaliyo bainishwa kweye rasimu ya Katiba mpya! Tusikubali propaganda za CCM, TUNATAKA SERIKALI TATU!

Naomba kuwasilisha!
 
Viongozi wa CCm wanajuwa wanakula vya mjinga kwa kumhadaa eti Serikali ya JMT ni serikali ya Tanganyika pia, huu ni uhuni usiovumilika. CCM wanachukulia udhaifu huo ndiyo ndiyo maana kila siku tunasikia wamefisadi huku na kule, sasa hivi wameingilia na biashara ya unga ili kutumaliza kabisa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…