CCM wasambaza waraka wao, wapinga rasimu ya Katiba Mpya

CCM wasambaza waraka wao, wapinga rasimu ya Katiba Mpya

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,575

Chama Cha Mapinduzi kimetoa mwongozo wake kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya, kikipinga mambo mengi yaliyomo ndani ya rasimu hiyo iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Mwananchi ambayo ina nakala kuhusu mwongozo huo wa CCM kwa wanachama wake, imebaini mambo mengi yaliyopendekezwa na tume ya Jaji Joseph Warioba ikiwemo muundo wa Serikali tatu yamepingwa na chama hicho tawala.

Kwa mujibu wa mwongozo huo ni kama vile CCM inataka kuendelea na Katiba iliyopo, kwa kuwa inaunga mkono mambo mengi ya katiba ya sasa na kupinga yaliyopendekezwa kwenye rasimu.

Mwongozo huo ulitolewa Juni 10 mwaka huu kwa baraka za mkutano wa Kamati Kuu (CC) ya Halmashauri kuu ya chama hicho kilichofanyika mjini Dodoma, ikiwa ni siku saba tangu Tume ya Mabadiliko ya Katiba kutoa Rasimu ya Katiba ambayo imeanza kujadiliwa na kutolewa maoni, kuanzia Julai 12 mwaka huu.

Katika mwongozo huo CCM kimeichambua Ibara ya 57-66 ya Rasimu ya Katiba inayoeleza kuwepo kwa mfumo wa Serikali tatu ambao utakuwa wa shirikisho linaloundwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Tanzania Bara.

Sura hiyo pia inaeleza kuwa shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na kusimamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Bunge la Jamhuri ya Muungano na Mahakama ya Jamhuri ya Muungano.

Katika mwongozo huo, CCM kinaeleza kuwa pendekezo hilo ni tofauti na sera ya chama hicho kuhusu muundo wa muungano wenye Serikali mbili ambazo ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

"Muundo huu wa Serikali mbili ulitokana na makubaliano na nchi mbili huru ambazo zilikuwa ni Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar mwaka 1964," inaeleza sehemu ya mwongozo huo na kuongeza;

"Inapendekezwa Jamhuri ya Muungano iwe ni nchi yenye muundo wa Serikali mbili. Kwa maana hiyo Ibara ya 57(1) na Ibara ya 57(3) (za Rasimu ya Katiba) ziondolewe ili shughuli za kiutendaji zinazohusu Tanzania Bara zisimamiwe na Serikali ya Jamhuri ya Muungano na zile za Zanzibar zisimamiwe na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar."

Kisheria, mwongozo huo unaeleza kuwa msingi mkuu wa muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar ni wa Serikali mbili kwa mujibu wa makubaliano ya mwaka 1964, kwamba mapendekeo ya rasimu hiyo yanafanya rejea ya makubaliano hayo.

"Mfumo wa Serikali tatu utaleta urasimu na utata wa kisheria katika umiliki na uendeshaji wa shughuli za kiuchumi na kijamii, pia kusababisha mgogoro katika uwakilishi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano kwani majimbo hayo yatakuwa mikoa kwa bara na mikoa kwa Zanzibar wakati uundwaji wa mikoa na wilaya si jambo la muungano," unaeleza mwongozo huo.

Kisiasa, mwongozo huo unaeleza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano itaelea kimadaraka na kimamlaka kwa sababu haitakuwa na uwezo wa kushughulikia moja kwa moja masuala yanayohusu wananchi kama elimu, afya, kilimo, maji, barabara kwa kuwa siyo mambo ya muungano.

Unaeleza kuwa kutokana na ukubwa wa eneo la uchumi wa Tanzania Bara ni wazi kwamba itachangia zaidi kwenye uendeshaji wa Serikali ya Muungano na kwamba jambo hilo linaweza kutoa mwanya kwa Serikali ya Tanzania Bara kuiburuza Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar.

Kiuchumi, mwongozo huo unaeleza kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano itakuwa tegemezi kwa Serikali zinazounda muungano hasa Serikali ya Bara ambayo itakuwa na uchumi mkubwa.

"Urasimu wa kibiashara na umilikaji ardhi utaongezeka kwa sababu biashara, ardhi na umilikaji mali wa aina nyingine si mambo ya muungano, pia gharama za uendeshaji wa Serikali uliopo ni mkubwa na kuwepo kwa Serikali tatu itakuwa gharama zaidi," unaeleza.

Kijamii, unaeleza kwamba Serikali tatu zitahatarisha amani, utulivu na utangamo wa kitaifa kwani watu wa pande mbili za muungano wamekuwa na uhusiano na mwingiliano kwa miaka mingi.

Katika sehemu ya faida za muundo wa Serikali mbili, mwongozo huo unafafanua kwamba muundo unaotumika sasa unawawezesha Wazanzibari kumiliki ardhi na rasilimali nyingine zilizopo Tanzania Bara kama raia wa Tanzania, ingawa ardhi na rasilimali nyingine za kiuchumi si masuala ya Muungano.

Katika mfumo wa kiutendaji kama ulivyoanishwa katika Ibara ya 67 hadi 101 ya rasimu hiyo, mwongozo huo unaeleza kuwa kutakuwa na mgongano wa viongozi pale ambapo Serikali hizo tatu zitakuwa chini ya uongozi wa vyama tofauti vya siasa au wagombea binafsi.

"Rasimu haijabainisha vyema mipaka ya uhusiano na ushirikiano kati ya Jamhuri ya Muungano na nchi au taasisi za nje kwa upande mmoja, kati ya Serikali ya Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na taasisi za nje.

"Hali hii inaweza kuleta mgongano kati ya Serikali hizi tatu, muundo wa Serikali hizi umeondoa nafasi ya Waziri Mkuu kuteuliwa kutoka miongoni mwa wabunge, lengo la Katiba iliyopo kutaka mawaziri wateuliwe kutoka miongoni mwa wabunge ni kuwafanya kuwajibika moja kwa moja bungeni ili Bunge liweze kuisimamia Serikali," unaeleza.

Hii ni mara ya pili kwa CCM kutoa mwongozo wa aina hiyo, kwani katika awamu ya kwanza ya kutoa maoni, chama hicho kiliandaa mwongozo wake uliojielekeza kwenye mambo makuu ya msingi na yenye masilahi pekee kwa taifa.

Hata hivyo, kati ya mambo hayo ni mawili tu ndiyo yaliyopo katika rasimu hiyo ambayo ni dola kutokuwa na dini rasmi pamoja na ukomo wa idadi ya wabunge.

Mambo ambayo yalitolewa maoni na chama hicho na kutokuingizwa katika Rasimu ya Katiba ni kuendelea kwa mfumo wa Serikali mbili, rais kupatikana kwa wingi wa kura, mawaziri kutokutoka nje ya Bunge, wajumbe wa NEC kuthibitishwa na Bunge.

Nyingine ni kutokuwepo kwa mgombea binafsi, kuendelea kwa viti maalumu bungeni pamoja na kutokuhojiwa kwa matokeo ya urais mahakamani.
 
CCM ni janga. walianzisha tume kuigopa CDM tu. Wananchi tusikubali mapendekezo hayo ya CCM kwani ni ya kishetani tu.
 
"Katiba sio sera ya chama fulani cha siasa katiba ni ya Watanzania wote" by Freeman Aikael Mbowe
 
Chama Cha Mapinduzi kimetoa mwongozo wake kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya, kikipinga mambo mengi yaliyomo ndani ya rasimu hiyo iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Kijamii, unaeleza kwamba Serikali tatu zitahatarisha amani, utulivu na utangamo wa kitaifa kwani watu wa pande mbili za muungano wamekuwa na uhusiano na mwingiliano kwa miaka mingi.

Katika sehemu ya faida za muundo wa Serikali mbili, mwongozo huo unafafanua kwamba muundo unaotumika sasa unawawezesha Wazanzibari kumiliki ardhi na rasilimali nyingine zilizopo Tanzania Bara kama raia wa Tanzania, ingawa ardhi na rasilimali nyingine za kiuchumi si masuala ya Muungano.

Natumai Watanganyika wanao Shabikia CCM huu ujumbe watakuwawameuona yaani kwa CCM Wazanzibari ndio muhimu kuliko sisi.

Katika mfumo wa kiutendaji kama ulivyoanishwa katika Ibara ya 67 hadi 101 ya rasimu hiyo, mwongozo huo unaeleza kuwa kutakuwa na mgongano wa viongozi pale ambapo Serikali hizo tatu zitakuwa chini ya uongozi wa vyama tofauti vya siasa au wagombea binafsi.

Kama nia yao ni kujenga Umoja wanahofu nini kuwe na Serikali moja?

"Hali hii inaweza kuleta mgongano kati ya Serikali hizi tatu, muundo wa Serikali hizi umeondoa nafasi ya Waziri Mkuu kuteuliwa kutoka miongoni mwa wabunge, lengo la Katiba iliyopo kutaka mawaziri wateuliwe kutoka miongoni mwa wabunge ni kuwafanya kuwajibika moja kwa moja bungeni ili Bunge liweze kuisimamia Serikali," unaeleza.

Nyingine ni kutokuwepo kwa mgombea binafsi, kuendelea kwa viti maalumu bungeni pamoja na kutokuhojiwa kwa matokeo ya urais mahakamani.

Kweli mfa maji haachi kutapatapa. Kwa Dunia ya leo unasimama jukwaani na kunadi kitu kama hii.Ni mwendawazimu na mafisadi waliopo na waliostaafu ndio wanaweza kukusifia na kukuunga mkono tu wengine wanaweza zimia kusikia hili na wasikusalimie tena !
 
CCM ni janga. walianzisha tume kuigopa CDM tu. Wananchi tusikubali mapendekezo hayo ya CCM kwani ni ya kishetani tu.
Sasa kwanini walikubali kwenda kwenye mchakato wa katiba mpya kama hawataki kubadilisha hii ya sasa maana wanachotaka ni status quo!

Cha msingi ni kumalizana nao kwenye kura ya rasimu ili wajue mapema kabisa kuwa 2015 hakuna anayewahitaji tena! Wakiangukia pua kwenye kura ya rasimu nadhani akili itawakaa sawa na watajiandaa kisaikolojia kushindwa 2015 maana sasa hivi hawatakikuamini kama watashindwa!
 
"Inapendekezwa Jamhuri ya Muungano iwe ni nchi yenye muundo wa Serikali mbili. Kwa maana hiyo Ibara ya 57(1) na Ibara ya 57(3) (za Rasimu ya Katiba) ziondolewe ili shughuli za kiutendaji zinazohusu Tanzania Bara zisimamiwe na Serikali ya Jamhuri ya Muungano na zile za Zanzibar zisimamiwe na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar."

Kisheria, mwongozo huo unaeleza kuwa msingi mkuu wa muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar ni wa Serikali mbili kwa mujibu wa makubaliano ya mwaka 1964, kwamba mapendekeo ya rasimu hiyo yanafanya rejea ya makubaliano hayo.
Akili gani hii? Shughuli za Tanganyika zisimamiwe na Muungano halafu za Zanzibar wasimamie wao? Hii kitu haiwezekani. Ndio maana hatuna wa kututetea Watanganyika. Dawa ni dola mbili huru. Tuwaache Wazanzibar wajifanyie mambo yao nasi twende na yetu. Why is it so hard to Let Tanganyika and Zanzibar Part?

Haya makubaliano ya 1964 yamekuwa obsolete. Yes, inawezekana yalikuwa mazuri at that time lakini kwa sasa hayana faida. Undugu wetu na Wazenj hauvunji kwa kutokuweo muungano. Tuachane kwa amani tu!

"Mfumo wa Serikali tatu utaleta urasimu na utata wa kisheria katika umiliki na uendeshaji wa shughuli za kiuchumi na kijamii, pia kusababisha mgogoro katika uwakilishi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano kwani majimbo hayo yatakuwa mikoa kwa bara na mikoa kwa Zanzibar wakati uundwaji wa mikoa na wilaya si jambo la muungano," unaeleza mwongozo huo.
Hii ni kweli lakini serikali mbili zimesha prove failure ndio maana ni heri, nasema tena ni heri tuachane kwa amani. Kama kukiwa na umuhimu wa kuungana tena si tutaongea kama tulivyoachana?

Katika sehemu ya faida za muundo wa Serikali mbili, mwongozo huo unafafanua kwamba muundo unaotumika sasa unawawezesha Wazanzibari kumiliki ardhi na rasilimali nyingine zilizopo Tanzania Bara kama raia wa Tanzania, ingawa ardhi na rasilimali nyingine za kiuchumi si masuala ya Muungano.
Huu ni upuuzi kabisa. Watanganyika wanapata nini? Na mbona Wazanzibari wanalalamika konewa?
Demolish the current system. Let Tanganyika and Zanzibar part!

Nyingine ni kutokuwepo kwa mgombea binafsi, kuendelea kwa viti maalumu bungeni pamoja na kutokuhojiwa kwa matokeo ya urais mahakamani.
Viti maalum: Dudu hili litatoka lini? Linanyonya kodi za wananchi bure!
Wabunge wote wawe wa kuchaguliwa. Hata wale wa kuteuliwa na Rais wasiwemo!
 
Back
Top Bottom