CCM wapiga marufuku takrima
Tausi Mbowe
CHAMA cha Mapinduzi (CCM), kimepiga marufuku wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya jumuiya zake na wapambe wao kwenda mikoani na wilayani kujinadi au kuwanadi wagombea
Naibu Katibu Kuu wa CCM (Bara), Kapteni George Mkuchika, alisema kuwa imebainika kuwa kuna vitendo vichafu vya rushwa vimeanza kufanywa na baadhi ya wagombea kwa lengo la kuwashawishi wajumbe wawapigie kura katika uchaguzi ujao.
"Wapo wagombea wanazunguka mikoani na wilayani kujitangaza wakati hata majina yao hayajateuliwa na vikao husika. Wakiwa huko hukutana na baadhi ya wajumbe na kuwapa takrima,"alisema na kuongeza:
"Wengine wanatumia wapambe na kuwagharamia kili kitu ili kufanikisha mipango yao ya kuingia madarakani kwa rusha".
Mkuchika alisema wagombea wengine wanapakana matope, kuwa kutoleana lugha chafu kwa lengo la kuchafuana, jambo ambalo ni kinyume na maadili ya chama hicho.
"Sisi katika CCM tunaamini kwamba viongozi wazuri na watakaoweza kukisaidia chama ni watakaochanguliwa bila rushwa, wanaochanguliwa na rushwa hawawezi kukisaidia chama kwasababu watashindwa kukemea rushwa, hivyo kuwa sehemu ya tatizo kwa jumuiya zao na chama," alisisitiza Mkuchika.
Mkuchika alisema ni marufuku wagombea na wapambe wao kujihusisha na vitendo vya rushwa ya aina yoyote pamoja na kutoa takrima au bahasha kwa wajumbe.
Alisisitiza kuwa ni marufuku kutumia lugha za kupakana matope katika kipindi chote cha mchakato hadi uchaguzi kwa sababu chama kinataka kuwa na viongozi safi.
Mkuchika aliwaonya wagombea watakaobahatika kuteuliwa kugombea nafasi mbalimbali kuheshimu dhamana waliyopewa na chama kwa kutojiingiza kwenye rushwa, vinginevyo atakayebainika atafutwa.
Alisema wagombea wote watapata nafasi ya kujieleza na kujinadi katika vikao vya uchaguzi kabla ya kupigiwa kula hivyo kujinadi nje ya vikao hivyo ni kosa.
Hii ni kauli nzito kuwahi kutolewa na CCM tangu kuanza kwa chaguzi mbalimbali ndani ya chama hicho.
Mkutano wa tatu wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM), kwajili ya kuchuja majina ya wagombea uongozi wa umoja huo kinatarajiwa kukutana kesho kutwa mjini Dodoma huku kukiwa na taarifa kuwa Kamati ya Utekelezaji iliyokutana mwezi uliopita chini ya Uwenyekiti wake Dk Emmanuel Nchimbi kuwaengua baadhi ya wagombea akiwemo Nape Nnauye anadaiwa kupewa alama 'E' kwa kigezo cha umri
Katika hatua nyingine mkataba wa ujenzi wa jengo la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), unaodaiwa kusainiwa kwa njia ya ufisadi umejadiliwa katika kikao cha Kamati Kuu ya CCM (CC) baada ya wanasheria wa chama hicho kuutiza upya mkataba huo.