Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Ally Hapi, amesema kuwa kero nyingi zinazowakabili wananchi zinatokana na baadhi ya watendaji waliopo kwenye nafasi mbalimbali kutotenga muda wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Akizungumza na wananchi wa Babati Mjini wakati akisikiliza kero zao, Hapi amewataka watendaji wa serikali kuacha kukaa ofisini na badala yake kushuka kwa wananchi ili kutatua changamoto zao zinazowakabili moja kwa moja huku akisisitiza kuwa kushindwa kufanya hivyo kunasababisha wananchi kukosa mahali pa kupeleka matatizo yao, hali inayowaacha wakilalamika bila msaada wowote.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Aidha, Hapi amesisitiza kuwa msingi wa CCM ni watu na haki, hivyo ni wajibu wa viongozi kuwajali na kuwathamini wananchi.
Amesema kuwa tabia ya kutosikiliza wananchi inachangia kuwafanya wakose mtetezi jambo ambalo linaweza kudhoofisha imani ya wananchi kwa serikali na Chama katika eneo husika.
Hapi amewataka viongozi na watendaji wote kuzingatia wajibu wao ili kuhakikisha changamoto za wananchi zinatatuliwa kwa haraka na kwa ufanisi.